30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI 97 CHUO CHA ARDHI WATUNUKIWA ZAWADI

Na AZIZA MASOUD-DAR ES SALAAM

CHUO Kikuu Ardhi (ARU), kimetoa zawadi kwa wanafunzi 97 baada ya kufanya vizuri katika mwaka wa masomo wa 2016/2017 na kati ya hao wasichana ni 53 na wavulana 44.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Naibu Makamu Mkuu wa Aru, Profesa Gabriel Kassenga, alisema kwa mwaka wa pili mfululizo sasa wasichana wamekuwa wakipata ufaulu mzuri ukilinganisha na wavulana waliopo katika chuo hicho.

“Tumetoa zawadi kwa wanafunzi bora  kitaaluma, wapo 97, kati ya hao wasichana ni 53 sawa na asilimia 55 na wavulana ni 44 sawa na asilimia 45, kwa mwaka mwingine tena wanafunzi wa kike wamechukua tuzo nyingi kuliko wa kiume,” alisema Profesa Kassenga.

Alisema zawadi hizo hutolewa kwa msaada wa wadau mbalimbali na zina lengo la kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine ili wafanye juhudi katika masomo waweze kupata ufaulu wa alama za juu.

Alisema katika zawadi hizo, mwanafunzi aliyetia fora ni Gloria Mtei aliyepata zawadi sita katika masomo tofauti.

Alizitaja zawadi zilizotolewa kuwa ni vyeti, fedha, vifaa vya kisasa vya kupimia ramani na nyumba, kompyuta mpakato na vifaa vingine vinavyohusiana na kozi walizosomea.

Mbali na zawadi hizo, alisema wanafunzi hao pia watapata fursa ya kuhudhuria  mikutano na kozi za programu wanazosomea katika nchi mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles