24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Walioguswa mradi wa EACOP Bukoba waridhishwa na fidia

Renatha Kipaka, Kagera

Baadhi ya wananchi walioguswa na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika Wilaya za Missenyi na Muleba mkoani Kagera,wamesema uhamisisho wa makazi na ardhi umesaidia kuwainua kiuchumi na kuwapa makazi ya kudumu ya kujengewa nyumba za kuishi.

Miongoni mwa waliguswa na mradi huo, Rehema Mahamudi na Respicus Kamgisha wamezungumza na Mtanzania Digital ilipowatembelea katika maeneo wanayoishi, wamesema hawakutegemea jambo hilo.

Kamgisha amesema mradi huo umepita kwenye shamba la miti ambalo kwa miaka zaidi ya saba amefanya kilimo hicho kwa kutengeneza maisha yake.

Amesema alipewa fidia kwa kuzingatia ukubwa wa shamba na eneo ambalo lilichukuliwa ambapo fedha aliyoipata aliweza kuitumia katika uwekezaji wa mbalimbali.

“Natumia fursa hii kuwashukuru wanaotekeleza mradi huu, shamba langu nilinunua kwa lengo la uwekezaji wa miti ambayo ingekuwa dhamana kwa hitaji langu hasa ninapotaka kukopa pesa kwenye benki,”amesema Kamgisha.

Naye Rehema Mahamudi kutoka Wilaya ya Muleba amesema wakati viongozi wa Kijiji na wahusika wa mradi wamefika kwenye makazi yake na kuhojiwa endapo anataka pesa au nyumba alichagua nyumba kwani mazingira ya nyumba yake hayakuwa yenye kuridhisha kuishi.

“Walivyoniuliza mama unataka nyumba au hela nikawambia nataka nyumba ya kukaa na wanangu kwani baba yao aliondoka kwa madai kwamba hali ya maisha ni ngumu nilikuwa nakaa nyumba ya nyasi chumba kimoja na watoto wote nane, “amesema Rehema.

Amesema baada ya kuhamia eneo hilo la nyumba ya vyumba vinne, jiko, choo, na maji hata afya za watoto wake zimeimarika.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi upande wa Tanzania, Catherine Mbatia amesema mradi haujaangalia uhamisho wa jamii bali hata ujenzi mbalimbali utakapoanza kufanyika vimewekwa vipaumbele ambayo vitatolewa kwa wananchi waliopo kwenye maeneo husika.

Amesema,vipaumbele ni nafasi ambazo hazihitaji utaalam mkubwa wenye kumfanya mwananchi ambaye hajasomea taaluma yoyote asikose kazi.

Ameongeza kuwa kwa upande wa Mkoa wa Kagera kuna waguswa 2196 kati ya hao waliojengewa nyumba ni 116 kwa wilaya ya Missenyi,Muleba,Bukoba vijijini,na Biharamulo.

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji( EWURA) Kanda ya Ziwa George Muhini amesema kwa jinsi ilivyo taratibu za uombaji vibali kwa wauzaji wa mafuta ya magari,depo za mafuta na wasafirshaji ndivyo inautaka mradi kufuata taratibu hizo.

Aidha EWURA imeangalia maombi ya vibali endapo yamekidhi vigezo ili waweze kufanya ufuatuliaji kwani shughuli itayofanyika kwenye mradi huo ni usafirishaji wa mafuta kwa njia ya mabomba.

Kwa mujibu wa tovuti ya EACOP ni kwamba mradi unaurefu wa km 1443 na kati ya hizo 296 zipo nchni Uganda ambapo bomba la mafuta ndipo litaanzia na 1147 upande wa Tanzania .

Mradi huo utapita kwenye mikoa minane ya Tanzania na ndani ya mikoa hiyo kutakuwa na vituo vya kuongeza msukumo wa mafuta ambapo viwili vitakuwa upande wa Uganda na vinne Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles