25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Riadha Walemavu kuondoka kesho

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Timu ya Taifa ya Riadha kwa watu wenye ulemavu inayowakilishwa na Mwanariadha, Sauda Njopeka, anatarajiwa kuondoka kesho kwa ajili kwenda kushiriki mashindano ya Dunia yatakayofanyika Machi 16, Mwaka huu nchini Tunisi.

Mashindano hayo ni kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kufuzu kushiriki Michezo ya Paralimpiki itakayofanyika Agosti, mwaka huu, Tokyo nchini Japan.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi bendera Machi 9 mwaka huu Rais wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania(TPC), Tuma Dandi, amesema Mwanariadha huyo atakwenda kushiriki kupangiwa daraja ambayo itafanyika Machi 12, Mwaka huu na baadaye kushiriki mashindano ya kusaka viwango vya kufuzu michezo ya Olimpiki.

Rais huyo amelishukuru Baraza la Michezo la Taifa kwa kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali yakiwamo viza,vifaa vya michezo,vipimo vya covid .

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wadau waliochangia kwa hali na mali kwa kutuwezesha kufanikisha hili,” amesema Dandi.

Naye Mwanariadha Njopeka amesema kuwa amewaahidi Watanzania wasubirie ushindi kwani amejiandaa vizuri .

Kwa upande wa Kocha, Bahati Mgunda, amesema mwanariadha huyo yupo vizuri na amemwandaa vyema na matumaini ya kwenda kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Naye Katibu Mtendaji wa BMT, George Msonde, amesema wanayofuraha kwa kukabidhi bendera timu ya Taifa ya riadha inayotarajia kuondoka Jumatano Machi 11, 2021 nchini Tunisia.

Ameongeza kuwa mwanariadha huyo ni mahili,ana uwezo hivyo hawana wasiwasi na Serikali inasubiri ushindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles