25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wakuu Idara za Uandishi vyuoni wapata somo sheria za habari

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) limesema vyombo vya Sheria kama mahakama havipaswi kufungwa na sheria ya habari katika kutoa hukumu yake kulingana na uzito wa kosa alilotenda Mwandishi wa Habari.

Kauli hiyo imetoewa leo Agosti 30, 2022 na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena mjini Morogoro wakati akizungumza na Wakuu wa Idara za Uandishi wa Habari kutoka Vyuo Vikuu na Vyuo vya Uandishi wa Habari nchini, katika warsha ya siku tatu kuhusu uandishi wa habari za uchunguzi zinazowahusu watoto.

Warsha hiyo imehusisha walimu na wakuu wa idara za uandishi wa habari katika kuwasaidia mikakati ya kuandaa na kuwa na waandishi wenye uwezo wa kuandika habari za watoto zenye tija kwa jamii.

Meena amesema, baadhi ya vipengele vya Sheria ya Huduma ya Habari ya Mwaka 2016, imelazimisha pale mwandishi atapobainika kuwa na kosa, basi afungwe si chini ya miaka mitatu.

‘‘Unapoweka sheria ya namna hii maana yake hakimu analazimishwa kumfunga mwandishi hata kama kosa lake halihitaji kifungo. Sio kila kosa linahitaji kifungo, makosa mengine unaweza kupewa onyo.

‘‘Lakini pia kwenye sheria hii, hakimu hapaswi kutoa kifungo cha miaka miwili, mmoja ama chini ya miezi sita. Pengine mwandishi kafanya kosa linalohitaji kifungo cha mwezi mmoja, kwa mujibu wa sheria hii ni lazima kifungo kianzie miaka mitatu. Hili halijakaa sawa,’’ amesema Meena.

Mjumbe huyo wa TEF amewaeleza wakuu hao wa idara kwamba, mhakato wa mabadiliko hayo ni mawazo ya taasisi nyingi nchini, na kwamba mapendekezo ya habari yamebeba mawazo ya taasisi zote 12 zilizoshiriki katika uandaaji wake.

‘‘Mchakato huu si wa TEF peke yake, ni muunganiko wa taasisi mbalimbali kwa uchache zikiwemo Twaweza, MISA-TAN, MCT, Jamii Forum.

Pia amewaeleza wakuu hao wa idara za habari kwenye vyuo vyao kwamba, nao ni sehemu ya Mchakato wa Mabadiliko ya Sheria ya Habari nchini.

‘‘Kama nilivyosema, Mchakato huu si wa TEF peke yake, ni muunganiko wa taasisi mbalimbali kwa uchache zikiwemo Twaweza, MISA-TAN, MCT, Jamii Forum.

‘‘Baada ya sheria hii kusainiwa na kuanza kutumika, wadau wa habari tulianza kuipinga ingawa kipindi kilichopita hatukupata ushirikiano kama ilivyo sasa,” amesema Meena.

Meena aliwapitisha walimu hao katika baadhi ya vipengele vilivyomo kwenye nakala ya Mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ikiwa ni pamoja na kuondoa utitiri wa vyombo vinavyosimamia tasnia ya habari.

Ameeleza kwamba, muundo wa vyombo vilivyoelekezwa na sheria iliyopo, unaweza kuvunjwa na kuunda chombo kimoja ambacho kitakuwa imara na kusimamiwa kisheri kama ilivyo katika taaluma nyingine nchini.

“Sheria inataja kuwepo kwa Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la Vyombo vya Habari na pia Mfuko wa waandishi. Kuwa navyombo vyote hivi vinavyofanya kazi ya aina moja, tunasema hapana.

‘‘Hapa tunashauri tuwe na chombo kimoja ambacho kitafanya kazi zote hizo kama ilivyo kwa taaluma za uanasheria, uhasibu, ukandarasi na nyingine ambao hawana utitiri wa vyombo,’’ amesema.

Pia amezungumzia hatua ya sheria kumpa mamlaka makubwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo kufungia vyombo vya habari kwa utashi wake.

‘‘Tunasema jambo hili halikukaa vizuri, kumpa mamlaka mtu mmoja kuamua hatma ya kazi za watu sio sawa. Mkurugenzi huyo akifunga chombo maana yake amefunga ajira lakini pi amewanyima haki wasomaji,’’ amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles