27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima Tabora wapewa miche 150,000 ya michikichi

Na Allan Vicent, Tabora

WANANCHI wilayani Kaliua mkoani Tabora, wameanza kunufaika na ahadi za Mbunge wao wa Jimbo la Kaliua ,Aloyce Kwezi baada ya kugawa miche 150,000 ya michikichi ili kuwahamasisha kulima zao hilo badala ya kutegemea tumbaku pekee.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara aliyofanya katika vijiji mbalimbali vya kata ya Ushokola wilayani humo jana na kusikiliza kero zao, amewataka kuchangamkia kilimo cha zao hilo kwa kuwa kitawapa manufaa makubwa.

Amesema zao hilo la kibiashara lina bei nzuri sokoni ambapo likishapandwa halimzuii mkulima kufanya shughuli zake nyingine za kiuchumi, hivyo akawataka wananchi kutenga maeneo ya kilimo hicho.

Ameeleza kuwa bei ya lita 20 ya mafuta ya mawese si chini ya  sh 60,000 na kuendelea, hivyo kama watalima zao hilo litasaidia kuongeza mapato na kuboresha maisha ya familia zao.

‘Nimewaombea miche zaidi ya 150,000 kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na tayari nimeshaleta miche 56,000 na kuigawa kwa wananchi, mingine 94,000 inakuja, mjitokeze kwa wingi kuichukua na muanze kuipanda’, amesema.

 Mkazi wa kijiji cha Ushokola, Mohamed Lukeleja (75), amekiri kuwa zao hilo lina manufaa makubwa kwa jamii, kwani  licha ya kuzalisha mafuta ya kupikia pia linatoa mazao mengine kama vile nta na mise ambayo yakichakatwa yanazalisha sabuni, gundi, lishe, mbolea, vifungo vya nguo na mengine mengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles