26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

WAKANDARASI WA MAJI WAPATA KIBANO KIKALI

Na Samwel Mwanga,

Simiyu

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameagiza wakandarasi waliolipwa fedha na Serikali
kujenga miundombinu ya maji wakashindwa
kuikamilisha kwa wakati wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Aweso ambaye ni mmoja wa mawaziri walioteuliwa hivi karibuni, alitoa maagizo hayo jana alipotembelea mradi wa ujenzi wa chujio la maji katika Bwawa la New Sola uliopo Kijiji cha Zanzui mkoani Simiyu.

Akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya PET Cooperation na Jossam & Company Ltd zinazojenga mradi huo,  alisema anasikitishwa na mradi huo kutokukamilika kwa wakati licha ya Serikali kuwalipa fedha zote.

Naibu huyo aliagiza hadi kufikia Desemba 30 mwaka huu mradi huo wa maji uwe umekamilika.

“Kitendo cha kampuni hizo kulipwa fedha na Serikali na kushindwa kukamilisha kazi hiyo kwa wakati hakivumiliki na nitachukua hatua kali dhidi ya kampuni zote nchini zitakazoendelea kufanya kazi kwa mazoea.

“Haiwezekani mkandarasi amelipwa kiasi chote cha fedha za kutekeleza mradi halafu wanashindwa kukamilisha kazi kwa wakati hata kama una mapembe marefu mimi kwa umri wangu huu mdogo nitakufuata huko huko ulipo na kuyakata mapembe hayo,”alisema Aweso.
Akizungumzia kukauka kwa Bwawa la New Sola ambalo ndicho chanzo kikuu cha maji katika Mji wa Maswa na vijiji vingine 11, Aweso alisema mbali
na  mabadiliko ya tabianchi shughuli za binadamu ndani ya bwawa hilo zimechangia kwa kiasi kikubwa kukauka na kusababisha kuwepo na shida kubwa ya maji katika mji huo.

“Hili bwawa limekauka kutokana na hali ya mabadiliko ya tabianchi lakini kwa asilimia kubwa limesababishwa na shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, ujenzi kuchungia mifugo zinazofanywa ndani ya eneo hili,” alisema.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira
Maswa (Mauwasa) Mhandisi Merchedes Anaclet alisema mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa mitambo ya kusukuma maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles