29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wajasiriamali wahimizwa uaminifu

Nathaniel Limu -Singida

 WAFANYABIASHARA, wajasiriamali wadogo na wakubwa mkoani Singida, wamehimizwa kudumisha uaminifu katika kurejesha mikopo kwa wakati, ili waweze kujijengea mazingira mazuri ya kuendelea kukopesheka na taasisi za kifedha.

Wito huo umetolewa jana na mfanyabiashara wa soko kuu mjini hapa, Samweli Lissu, wakati akichangia katika hafla ya kutoa mikopo kwa wajasiriamali 15.

Mikopo hiyo yenye thamani ya Sh milioni imetolewa na SIDO mkoani hapa.

Lissu alisema uaminifu ni sifa pekee ambayo itamsaidia binadamu aweze kuishi maisha mazuri, na yasiyo na misukosuko.

“Mkopaji akiwa mwaminifu kwa kurejesha mkopo kwa wakati, atajijengea sifa ya kuendelea kukopeshwa zaidi na zaidi. 

“Pia kwa kurejesha mkopo kwa wakati, ataiwezesha taasisi ya kifedha kukopesha wateja wengine wapya,” alifafanua.

Aliwahimiza waendelee kulipa kodi/ushuru wa Serikali kwa wakati. Sambamba na ulipaji kodi ya Serikali, aliwataka vile vile wakumbuke kulipa au kutoa sadaka asilimia 10 ya mapato yao kwa muda husika.

“Tukimtolea Mungu sehemu yake, Mungu atabariki biashara zetu za aina mbalimbali kuwa na tija zaidi, na biashara zitakuwa endelevu.

“Tutakapokuwa tunalipa kodi ya Serikali, tujue pia tunalazimika kutoa sadaka ya asilimia 10  ya mapato yetu  kwa Mungu wetu.

“Kwa sisi wafanyabiashara wadogo, mkombozi wetu ni Sido, haina masharti magumu. Mimi nina nyumba yenye thamani ya milioni 40, nimeenda benki moja hapa mjini kwetu, wameninyima mkopo,” alisema Lissu.

Naye mfanyabiashara  mwingine wa soko kuu, Agnes Tarimo, alisema ili kuharakisha kuboresha miradi yao, ni lazima wakimbilie taasisi za kifedha.

“Hawa ndugu zetu wapo vizuri zaidi. Sijasikia wameuza nyumba ya mkopaji. Wamewasimamia vizuri wakopaji hadi kumaliza mkopo,” amefafanua.

Katika hatua nyingine, Ofisa  Mikopo wa Sido Mkoa wa Singida, Rubein Mwanja,  amesema wao ni wasikivu na hawana ubaguzi wa aina yoyote katika kutoa mikopo.

“Kukopa  ni rahisi, hatuna masharti magumu  kwa mfanyabiashara au mjasiriamali kupata mkopo. Masharti yetu ni nafuu… mali yako ya ndani au hata biashara yako,  tukiiona imekaa vizuri tunakupa mkopo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles