24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wagonjwa 70 kuzibuliwa mishipa ya damu JKCI

 

VERONICA ROMWALD NA FRANK KAGUMISA (SAUT)- DAR ES SALAAM

WATU 70 wanaokabiliwa na tatizo la kuziba mishipa ya damu (Coronary Artery Disease) watafanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa yao katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),.

Akizungumza na MTANZANIA hospitalini hapo jana, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo JKCI, Peter Kissenge, alisema  upasuaji huo utafanyika Septemba 29, hadi Oktoba 10.

Tutashirikiana na wenzetu kutoka Shirika la Albasam Charity Organization la   Saudi Arabia kufanya upasuaji huu.

Tunawasihi madaktari katika hospitali nyinginezo kote nchini kuwapa rufaa wale aliobainika kuwa na tatizo hili kuanzia sasa hadi  Septemba 26.

“Hatua hiyo itatuwezesha kuwafanyia uchunguzi wa awali kwa wakati  kujua aina gani ya matibabu wanastahili wagonjwa husika na kuwapangia ratiba ya siku ya upasuaji,” alisema.

Dk. Kissenge alisema tathmini iliyofanyika tangu   upasuaji wa aina hiyo uliopoanza katika taasisi hiyo, inaonyesha matatizo ya moyo nchini yanazidi kuongezeka hasa kwa watoto.

“Hii inasababishwa zaidi na mtindo mbovu wa maisha, ulaji usiofaa hasa vyakula vyenye chumvi na mafuta mengi na hata kutokufanya mazoezi.

“Hivyo tunawasihi wananchi waepukane na hayo  kujikinga na magonjwa haya,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles