31 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wagombea waliorudishwa na NEC kuwania ubunge sasa wafika 28

Faraja Masinde -Dar es salaam

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imerejesha wagombea ubunge wengine 13 waliokuwa wameenguliwa na kufanya idadi ya waliorudishwa kwenye kinyang’anyiro hicho  kufikia 28 ikiwa ni baada ya juzi kutangaza wengine 15 waliorudishwa kugombea.

Jana NEC, ilitoa taarifa kwa umma iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Charles, ikisema imekubali rufaa 13 na kuwarejesha wagombea katika orodha ya wagombea.

 “Rufaa hizo ni kutoka kwenye majimbo ya Singida Magharibi, Madaba, Ilemela, Namtumbo, Bagamoyo, Liwale, Tunduma, Bukene na Kigamboni,” ilisema taarifa hiyo.

Ilieleza kuwa imekataa rufaa saba za wagombea ambao hawakuteuliwa, ambazo ni kutoka majimbo ya Singida Magharibi, Bahi, Handeni Vijijini, Madaba, Singida Mashariki, Ileje, Meatu na Bukene.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, NEC pia imekataa rufaa 14 za kupinga walioteuliwa kutoka majimbo ya Mwanga, Mafinga, Ilala, Manonga, Igunga na Kisesa.

 “Idadi hii inafanya rufaa za wagombea ubunge zilizofanyiwa uamuzi na NEC kufikia 89, hii inafuatia taarifa kwa umma iliyotolewa Septemba 8 ambapo tume ilitangaza uamuzi wa rufaa 55.

“Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku. Wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa tume,” ilisema taarifa hiyo.

MCHANGANUO WALIOREJESHWA JUZI

Wagombea ubunge ambao rufaa zao zimekubaliwa na kurejeshwa na NEC juzi ni pamoja, Madoga Aisha Saleh ambaye ni mgombea wa Chadema Dodoma Mjini, Kurwa Lubuva mgombea wa Chadema Kibiti na mgombea wa Jimbo la Mkwajuni kwa tiketi ya NCCR Mageuzi, Pandu Haji Sheha.

Mwingine ni mgombea wa Jimbo la Gando kwa tiketi ya ADA Tadea, Ramadhani Abdallah Ramadhan, mgombea wa Jimbo la Nyamagana kwa tiketi ya NRA, Paul   Soleji, mgombea wa Jimbo la Vwawa kwa tiketi ya Chadema, Fanuel Mkisi na mgombea wa Jimbo la Handeni Vijijini kwa tiketi ya CUF, Bashiri Muya.

Mgombea wa Jimbo la Kijijini kwa tiketi ya Chadema, Mize Ali Haji, mgombea wa Jimbo la Wingwi kwa tiketi ya CUF, Ali   Othman Ali,

mgombea wa Jimbo la Tumbe kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Khamis Ali Omar na mgombea wa Jimbo la Nungwi kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Ame Is-haka Sheha.

Wengine ni mgombea wa Jimbo la Chaani kwa tiketi ya Chadema, Juma Haji Sauti, mgombea wa Jimbo la Mpanda Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Kisesa Michael na mgombea Jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya ADC, Rehema Swalehe Mjengi.

RUFAA ZILIZOKATALIWA

Kwa mujibu wa taarifa ya NEC, rufaa zilizokataliwa ni 23 ambazo ni za mgombea wa Jimbo la Manyoni Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Aisha Luja, rufaa ya mgombea wa Jimbo la Kojani kwa tiketi ya CCM, Hamad Hassan Chade, rufaa dhidi ya mgombea wa Jimbo la Kondoa kwa tiketi ya CCM, Dk. Ashatu Kijaji, rufaa dhidi ya mgombea wa Jimbo la Chaani kwa tiketi ya CCM, Juma Hamad na rufaa dhidi ya mgombea wa Jimbo la Pandani kwa tiketi ya CCM, Abdallah Rashid Othman.

Nyingine ni rufaa dhidi ya mgombea wa Jimbo la Mkoani kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Khamis Mohammed Khamis, rufaa dhidi ya mgombea wa Jimbo la Wingwi kwa tiketi ya CCM, Omar Issa Kombo, rufaa dhidi ya mgombea wa Jimbo la Tumbe kwa tiketi ya CCM, Amour Khamis Mbarouk.

Nyingine ni ya mgombea wa Jimbo la Konde kwa tiketi ya CCM, Sheha Mpemba Faki, rufaa dhidi ya mgombea wa Micheweni kwa tiketi ya CCM, Abdi Hija Mkasha.

Pia rufaa nyingine iliyokataliwa ni dhidi ya mgombea wa Mtambwe kwa tiketi ya CCM, Mgeni Khatib Yahya, rufaa dhidi ya mgombea wa Jimbo la Mtambile kwa tiketi ya CCM, Khamis Salum Ali.

Pia rufaa dhidi ya mgombea wa Jimbo la Kiwani kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Omar Ali Mzee.

AMBAO HAWAJATEULIWA

Aidha, katika hatua nyingine NEC haijawateua baadhi ya wagombea ubunge kuwania nafasi ya ubunge kwenye majimbo mbalimbali.

Wagombea hao ni pamoja na Askofu Mussa Samsoni Mlawi aliyekuwa akiwania jimbo la Dodoma Mjini kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Mtumwa Haji Makame aliyekuwa akiwania Jimbo la Tumbatu kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Salvatory Sege aliyekuwa akiwania Jimbo la Kilosa kwa tiketi ya Chadema na Edson D’zombe aliyekuwa akiwania Jimbo la Lupembe kwa tiketi ya Chadema.

Pia wamo Msabaha Rajabu aliyekuwa akiwania Jimbo la Kilosa kwa tiketi ya CUF, Sabahi Khamis Abdallah Abdullah aliyekuwa akiwania Jimbo la Paje kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Khamis Moh’d Nassor aliyekuwa akiwania Jimbo la Kijini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Mzee Saleh Abdallah aliyekuwa akiwania Jimbo la Wawi kwa tiketi ya ACT na

Mzee Saleh Abdallah aliyekuwa akiwania Jimbo la Wawi kwa tiketi ya ACT.

Wengine ni pamoja na Felix Marcus aliyekuwa akiwania Jimbo la Dodoma Mjini kwa tiketi ya DP,

Suleiman Khalfan Said aliyekuwa akiwania Jimbo la Ole kwa tiketi ya ACT, Bakari Hassan Hamad aliyekuwa akiwania Jimbo la Kojani kwa tiketi ya AAFP, Khalifa Mohammed Issa aliyekuwa akiwania Jimbo la Mtambwe kwa tiketi ya ACT.

 Pia yumo Mwandi Robert Athuman aliyekuwa akiwania Jimbo la Rungwe kwa tiketi ya NCCR Mageuzi, Dk. David Mallole aliyekuwa akiwania Jimbo la Dodoma Mjini kwa tiketi ya ACT, Idrisa Omar Haji aliyekuwa akiwania Jimbo la Mkoani kwa tiketi ya NCCR, Ndesamburo Philemon aliyekuwa akiwania Jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya Chadema na Ndesamburo Philemon aliyekuwa akiwania Jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya Chadema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles