24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wafungwa wengi wanakosa mawakili-Tume

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

MWENYEKITI wa Tume ya Haki ya Jinai, Jaji mstaafu Mohamed Chande Othman, amesema bado wanafanya uchambuzi kwani wamebaini kuwa watuhumiwa wengi wa makosa ya haki jinai wanahumkumiwa na kutiwa hatiani kwa adhabu za kifungo cha miaka mingi kuanzia 30 mpaka maisha bila kuwa na wakili.

Akizungumza leo Mei 2, jijini Dar es Salaam Jaji Othman katika mkutano ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje uliowakutanisha Tume, Mabalozi na Wakuu wa Taasisi za kimataifa yaliyopo nchini amesema lengo ni kuwapa taarifa na madhumuni ya tume hiyo.

“Mtuhumiwa hana utetezi, hawajui sheria, hawajui kiingereza na wakati mwingine kesi zinaenda mpaka rufaa. Je hawa wapate msaada wa kisheria kutoka kwa nani? na kwa mfumo gani? kwa hiyo mambo mengi yako mbele ya tume ndio tupo kwenye hatua ya uchambuzi lakini hatufungi mlango, kuna taasisi ambazo zitakuwa tunaziita tunazihoji na nyingine ziataendelea kutoa maoni,” amesema Jaji Othman.

Amesema tume hiyo ilianza kazi mosi, mwaka huu, kwa kipindi cha miezi kitatu imefanikiwa kuwahoji wananchi 10,000, mikutano 25 na wilaya 53.

“Tumeona ni muda muafaka wadau wengine ambao ni nchi zilizopo Tanzania zenye mashirikiano na haki hasa za umoja wa mataifa na wao wapate taarifa ya mwendelezo wa shughuli yetu, maadhumuni na majukumu ya tume na mbinu tunazotumia kukusanya takwimu na taarifa na hatua tuliyofikia,” amesema Jaji Othman.

Ameongeza kuwa tume hiyo itaangalia uzoefu mzuri wa nchi nyingine ambazo zinafanya maboresho ya haki jinai hasa kwa walewaliofanikiwa kama yatafaa kwenye mazingira yetu.

Aidha, amesema mbeleni inawezekana kuna maeneo ambayo watataka kujumuika na hizo taasisi kushirikiana hivyo wamebadilishana nao mawazo.

Jaji Othman amesema mchakato wa kuangalia mambo mengine bado unaendelea na wako kwenye hatua ya uchambuzi nakwamba wamesikia mambo mengi lakini hawafungi mlango huku akisisitiza kuwa kuna wengine wataitwa kutoa maoni.

Alisema uchambuzi wamejiwekea wiki nne za kufanya uchambuzi na pia kuandaa rasmi ya mwanzo ya mapendekezo na nia yao ni kuwa na mapendekezo ya aina kadhaa yakiwamo yale ambayo hayana muda wa kusubiri.

Nae, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab, amesema tume kama hiyo imekuwa z.ikianzishwa tangu uhuru wa Tanganyika na maboresho mbalimbali yamefanyika ikiwa ni matokeo ya tume hizo.

“Dhamira ya Serikali kuhakikisha kunakuwepo na mifumo imara ya haki jinai na tume hii tunatarajia ije na mapendekezo yatakayoboresha mfumo wa haki jinai kulingana na mahitaji ya sasa,” amesema Balozi Fatma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles