Kinshasa, Kongo DRC
Wakati hali ya dharura katika mikoa ya Kivu ya Kaskazini pamoja na Ituri inaingia siku yake ya tano tangu kutangazwa na rais wa Tshisekedi, wanajeshi wa DRC wamekabiliana na waasi wa ADF katika mji mdogo wa Halungupa.
Taarifa zinasema kwamba waasi kumi waliuawa na silaha zao sita kukamatwa na jeshi. Na wakati huo huo, kuna ujumbe wa jeshi la Uganda uliowasili Beni,katika maandalizi ya operesheni za pamoja kati ya jeshi la Uganda na lile la Kongo.
“Tumeona na kuhesabu maiti kumi ya wapiganaji wa ADF na kukamata silaha ya kawaida AK-47,” alisema Meleki Mulala, msemaji wa jeshi la Kongo.
Hatua hiyo imepokelewa kwa shangwe kubwa na mashirika ya kiraia ya Sekta ya Ruwenzori kwa namna ya pekee na yale ya wilaya na mji wa Beni kwa ujumla. Majeshi ya Kongo yanasema yana uwezo wa kupambana na ADF
Akizingumza na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW), baada ya kuona maiti za waasi wa ADF kumi waliouawa Halungupa, Meleki Mulala, mwenyekiti wa mashirika ya kiraia maarufu Nouvelle société civile katika sekta ya Ruwenzori,pamoja na kushangaa kuona miili ya ADF, anawaomba wakaazi kuliunga mkono kikamilifu jeshi la Kongo,ili kuhakisha kwamba amani ya kudumu inarudi katika Sekta ya Ruwenzori. Huyu hapa Meleki Mulala.