Na Sheila katikula, Mwanza
Waajiri wameombwa kuunga mkono vita dhidi ya rushwa ya ngono sehemu za kazi kwa kijiepusha kujiepusha na vitendo hivyo  kwa wafanya kazi wao pindi wanapokwenda  kuomba  ajira kwenye ofisi zao.
Akizungumza kwa niaba ya Waandishi wa Habari Wanawake  kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake dunia yaliyofanyika wilayani Magu mkoaniÂ
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la waandishi wa habari za Utalii Kanda ya Ziwa, Rose Jacob, wakati wa maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliyobeba kauli mbiu ya Wanawake katika uongozi chachu ya kufikisha dunia yenye usawa.
Alisema ni vyema waajiri pamoja na wanamke kukemea  vitendo vya gono kazini kwani ni lazima  kila mtu kujiona wa thamani muda wote sanjari na kujitambua kujiheshimu, kujiamini na kupinga changamoto hiyo kazini.
“Ninaamini mtu akijitambua yeye ni nani na ana thamani gani kwenye jamii hawezi kulifumbia macho suala hili na badala yake  pindi atakapikutana na changamoto hiyo ni vema akatowe taarifa kwenye vyombo vya dola ili waweze kumchukulia sheria mhusika.
“Nawaomba waandishi wa habari wasikubali kutoa miili yao kwa ajili ya kupatiwa ajira,jambo ambalo linasababisha kutoku heshimika na kudhalilika kwa wanawake ikiwa na kupoteza ajira hiyo uliyoipata kwa ajili ya kutoa ngono,”alisema Rose.
Katika maadhimisho hayo waandishi wa habari wanawake mkoa wa Mwanza waliitumia siku hiyo kutembelea kiwanja cha Chama cha Waandishi wa habari mkoani Mwanza (MPC) kilichopo wilayani Magu mkoani Mwanza ambako zitajengwa ofisi za chama hicho.
Aidha, katika Maadhimisho hayo waandishi hao walifanya harambe na kukusanya mifuko  ya Saruji 100 ambayo itasaidia kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ofisi ya Chama cha Waandishi wa Habari mkoani hapaÂ