30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wakubwa waanza kuonesha njia, wakubali kuhama Ngorongoro

Na Mwandishi wetu, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela  ametaja majina ya Viongozi wakubwa wa kwanza waliokubali kuhama katika  Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni mkoani Tanga kuungana na wananchi wengine ambao wameshahamia. 

Ameweka wazi majina hayo leo Juni 28, 2022 jijini Arusha wakati  akizungumza na Waandishi wa Habari kuelezea tathmini ya  muendelezo wa awamu ya tatu ya  wananchi waliokubali kuhama katika eneo hilo na kwamba kundi hilo lenye kaya 25 litaanza safari Alhamisi ya wiki hii.

Kapteni wa Jeshi Mstaafu na  ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya awamu ya nne, Kaika Ole Telele akiwa ameshikilia bango wakati tathmini ikifanyika katika moja ya nyumba zake kwa ajili ya kulipwa fidia mara baada ya kukubali kuhama kwa  hiari katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kupisha shughuli za uhifadhi.

Ametaja majina hayo akiwemo aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Jimbo Ngorongoro Mkoani Arusha, Mhe. Kaika Ole Telele, Diwani wa kata ya Eyasi, Augustino Lukumay, Diwani wa Viti maalum wa Kata ya Eyasi, Veronica Litiga pamoja na Kiongozi wa Kabila la Wadatoga.

Mongela amesema hatua hiyo inaleta matumaini makubwa katika mchakato huo na kubainisha kuwa Viongozi hao kwa pamoja wamekiri kuwa wapo tayari kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera kwa lengo la kupisha shughuli za Uhifadhi.

Ameongeza kuwa viongozi hao ambao wamekuwa na ushawishi mkubwa katika jamii hiyo wamesema ikiwa wao ni viongozi wameamua kuchukua uamuzi huo ili kuonesha njia kwa wananchi wengine ili waanze kujitafakarikuhama katika eneo hilo lenye maslahi makubwa kwa  taifa.

Kwa upande wake Kapteni wa Jeshi Mstaafu na ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya awamu ya nne ameeleza kuwa ameamua kufanya maamuzi ili kuonesha yeye sio kikwazo katika mpango huo wa serikali wa kuhamisha wananchi kwa hiari.

Nae Diwani wa Kata ya Eyasi, Augustino Lukumay ameeleza uamuzi huo wa serikali ni wa busara na kwamba ni muda muafaka kwao wananchi wa Ngorongoro kuanza kumiliki nyumba, ardhi na kujishugulisha na shughuli za kiuchumi ambazo tokea kuzaliwa kwao Ngorongoro hawakuwahi kuzipata ila kwa sasa Msomera wanakwenda kuwa na haki hizo kama ilivyo kwa watanzania wengine.

Diwani wa viti maalum wa Kata ya Eyasi, Veronika Litiga amelezea kuwa yeye kama kiongozi ameamua kuonesha njia na kwamba hatua hiyo ya serikali ya kuhama kwa hiyari katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni moja ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi na kwa kuwa yeye ni mwanachama wa chama hicho ni lazima aweze kuitikia wito huo wa serikali

”Ninakwenda Msomera nikiwa na amani kwa vile naamini Chama changu na serikali yangu haiweze kunipeleka mahali ambako ni kubaya naamini Msomera ni mahali bora kwa ajili ya wanangorongoro walioteseka kwa muda mrefu kwa kukosa haki ya kuendesha shghuli za kiuchumi katika eneo la Uhifadhi,” amesema Litiga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles