29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

UWANJA WA NDEGE MWANZA KUKAMILIKA MWAKANI

Na JUDITH NYANGE -MWANZA

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa,  amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha  mradi  wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza unakamilika ifikakapo Julai  mwaka 2018.

Akizungumza juzi  wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua shughuli za ujenzi wa uwanja huo, Kwandikwa  alisema ameridhishwa na kasi ya ujenzi inavyoendelea na lengo la Serikali ni kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

Alisema amefanya mazungumzo na wataalamu wa ujenzi wa uwanja huo  na wamemhakikishia kuwa mazingira ya kazi yakiwa mazuri wanaweza kukamilisha kabla ya Julai mwaka 2018, hivyo wananchi wa Mwanza na mikoa jirani wategemee kupata huduma nzuri.

“Kukamilika kwa mradi huu mapema kunafanya huduma za ujenzi zisiongezeke, kama tutachelewa kumaliza gharama za ujenzi zinaweza  zikaongezeka na kuwanyima wananchi huduma na maendeleo yao,” alisema Kwandikwa.

Akizungumzia suala la malipo ya mkandarasi wa uwanja huo, Kwandikwa alisema kuna uhusiano mdogo kati ya malipo na ujenzi hivyo mkandarasi huyo anaweza kutafuta mkopo ili aweze kufanya kazi yake na kuendelea kulipwa kadiri  fedha zinavyopatikana na hana mashaka naye kutokana na nguvu aliyonayo.

“Mkandarasi anajua atapata fedha ndiyo maana kwa sasa hali ya mradi inakwenda vizuri, tunatamani ukamilike kabla Julai mwaka 2018, ni kweli wanahitaji fedha ili kufanya kazi  na sisi kwani hali ya fedha kwa sisi inaendelea kuwa nzuri,” alisema Kwandikwa.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, David Matovola, alisema baada ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa uwanja huo kukamilika, awamu ya pili itahusisha ujenzi wa jengo la abiria ili liweze kufanana na hadhi ya kiwanja hicho pamoja na mipango ya Serikali ya kuboresha sekta ya uchukuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles