27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Uhusiano wa kula matunda na furaha ya mtu

matunda

Na William Shao,

Uliaji wa matunda na mboga za majani unaweza kukusaidia kupata furaha, utafiti mmoja wa Australia umegundua.

Watafiti hao wamegundua kuwa watu waliobadili mtindo wao wa ulaji, na kuanza kula matunda na mboga za majani kwa wingi katika mlo wao wa kila siku wamepatwa na ongozeko la kuwa na hisia za furaha na kuridhika kimaisha “kwa namna ile ile ambayo mtu asiye na ajira anavyohisi mara apatapo ajira,” likasema jarida “American Journal of Public Health’.

“Ni wazi kuwa ulaji wa matunda na mboga za majani huongeza furaha yetu kwa kasi zaidi kuliko inavyoongezeka kutokana na afya ya mhusika,” anasema Redzo Mujcic, ambaye ni mtafiti mwenza wa ‘afya ya uchumi’ katika Chuo Kikuu cha Queensland nchini Australia.

Utafiti uliofanyika kabla ya huo ulionyesha kwamba kula mboga na matunda mengi kumesaidia mno kuimarisha sana afya ya miili ya watu, lakini faida kama hizo zinaanza kuonekana baada ya kipindi kirefu cha wakati, wanasema watafiti hao.

“Motisha wa watu kula vyakula vyenye afya kulidhoofishwa na ukweli kwamba faida za kuwa na afya ya mwili, kama vile kujikinga dhidi ya saratani, kuliongezeka miongo kadhaa baadaye,” akasema Mujcic. Kwa upande mwingine, kisaikolojia afya ya mwili inaimarika mapema zaidi.

Gazeti ‘Daily Mail’ Julai 11, 2016 liliandika hivi: “Kwa muda mrefu ilifikiriwa kuwa ulaji wa matunda na mboga mboga ni mzuri kwa afya yako, lakini sasa inaonekana ulaji huo unaweza kukupa furaha pia.”

Utafiti huo walifanyiwa watu 12,000 nchini Australia, ambao tabia zao zilifuatiliwa kwa miaka miwili. Hatimaye, linasema ‘Daily Mail’, iligundulika kuwa “…kadiri tulapo matunda kwa wingi zaidi, ndivyo tunavyokuwa na furaha zaidi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles