30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

UGONJWA WA TYPHOID NA MATIBABU YAKE

UGOJWA wa homa ya matumbo maarufu kama typhoid husababishwa na bakteria aina ya  salmonella typhi,ugonjwa husumbua zaidi nchi zinazoendelea.

Mara chache typhoid husababishwa na bakteria mwingine aitwaye salmonella paratyphi ingawa huyu  huwa hasababishi maradhi makubwa kama yule wa kwanza.

Bakteria hawa hupatikana katika kinyesi ambapo huambukiza na typhoid  kwa kupitia chakula au maji yaliyochafuliwa na kinyesi ama kugusana na mtu mwenye typhoid.

Katika nchi nyingi zinazoendelea zenye mlipuko wa typhoid, maambukizi hutokana na maji yaliyochafuliwa na kinyesi na hii huchangiwa na  kuwa na utaratibu mbovu wa kuondoa majitaka.

Katika nchi hizi  waathirika wengi ni wasafiri ambao baadaye huwaambukiza wenzao kwa njia njia ya kinyesi kwenda kinywani.

Maana yake ni kwamba, bakteria hawa huishi ndani ya kinyesi au mara myingine katika mkojo wa mtu aliyekwisha ambukizwa.

Unaweza kuambukizwa kwa kula chakula kilichoshikwa na mtu mwenye maambukizi ikiwa mtu huyo hakuosha vizuri mikono yake baada ya kwenda haja kubwa. Unaweza pia kuambukizwa wadudu hao kwa kunywa maji yanye vijidudu hao.

Wasambazaji wa Typhoid

Watu wengine (wachache) waliokwisha pata maambukizi wakatibiwa, bado huwa na wadudu hawa wakiwa wamejificha ndani ya utumbo wao au vifuko vyao vya nyongo kwa miaka mingi.

Watu hawa huendelea kutoa bakteria kutoka kwenye vinyesi vyao na kuwaambukiza watu wengine, ingawa wao wenyewe hawataonyesha dalili zo zote za kuwa na typhoid. Watu hawa huitwa “chronic carriers” au wasamabazaji wa typhoid.

Madhara ya typhoid 

Madhara makubwa ya typhoid ni kutokwa na damu au kutoboa vijitundu katika utumbo,hali hii  inaweza kukutokea wiki tatu baada ya kupata maambukizi ya bakteria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles