32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

UGANDA YAZUIA MATANGAZO YA ‘LIVE’ BUNGENI

KAMPALA, UGANDA

VITUO vya televisheni na redio vilivyokuwa vikitangaza matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni kujadili mabadiliko ya Katiba jana vilikatiza matangazo kufuatia amri kutoka Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC).

Ukatizaji huo unatokana na amri ya Septemba 26 iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa UCC, Godfrey Mutabazi ikivitaka vituo vyote kusitisha matangazo ya moja kwa moja kwa kile alichosema yanachochea umma, chuki na kuhamasisha utamaduni wa machafuko miongoni mwa watazamaji na kuhatarisha usalama na machafuko.

Hata hivyo, baadhi ya wachangiaji katika mitandao ya kijamii, wamevishangaa vyombo vya habari bungeni kwa kuitii amri hiyo, ambayo inaweza kupingwa mahakamani.

Mmoja wa watumiaji wa Facebook ajulikanaye Doreen Nyanjura alisema: “Inashangaza kuona vyombo vya habari vinapewa amri ya kipuuzi, vinaitii mara moja, ajabu sana, vinatakiwa kuipinga mahakamani,” alisema.

Mchangiaji mwingine katika Facebook Mayimuna Nabagereka aliandika: “Marufuku ya UCC dhidi ya matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni ni hadi pale Rais wa maisha atakapopitishwa kwa kuondoa ukomo wa umri.

Mchangiaji huyo alimlenga Rais Yoweri Museveni, ambaye yuko katika harakati za kuhakikisha Katiba haimzuii kuendelea kuongoza taifa hilo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Taifa cha Watangazaji Uganda (NAB), Bill Tibaigana, alisema wao wamejipanga kutoa kauli kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, Tume imesema haitasita kutoa adhabu kali iwapo amri yake itakiukwa ikiwamo kusimamishwa, kufutwa leseni kwa mujibu wa kifungu namba 41 cha Sheria ya Mawasiliano ya Uganda 2013.

Wabunge na Waganda wengine wamegawanyika vikali juu ya hoja ya kufuta Ibara 102 (b) kutoka Katiba ya Uganda, ambayo inazuia watu wenye umri zaidi ya miaka 75 kuwania urais.

Mpango huo unalenga kumwezesha Rais Museveni (73) aliye madarakani kwa miaka 31 sasa kuwania urais mwaka 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles