25 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Udhalilishaji makarani wa sensa wakemewa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakati Serikali ikiongeza muda wa siku saba kukamilisha zoezi la sensa ya watu na makazi, wananchi wameonywa kuacha tabia ya kuwadhalilisha makarani wa sensa.

Mkurugenzi wa Shirika la Sauti ya Jamii Kipunguni, Seleman Bishagazi, akizungumza na wanajamii kutoka makundi mbalimbali kukemea udhalilishaji wa makarani wa sensa.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Anna Makinda, amesema hadi kufikia Agosti 29, 2022 kaya zilizohesabiwa ni asilimia 93.45 na kwamba wameamua uongeza muda.

Wakizungumza leo Agosti 30, 2022 wakati wa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa mashirika, viongozi wa vikundi na wafanyakazi wa majumbani yaliyoandaliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Sauti ya Jamii Kipunguni (SAJAKI), baadhi ya washiriki wamesikitishwa na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya makarani hasa wanawake.

Mmoja wa washiriki Lyvia Mhagama, amesema baadhi ya makarani hawaaminiki wanaonekana ni dhaifu na kushauri waambatane na wajumbe.

Mshiriki mwingine Vida Philipo amewashauri makarani kuzingatia mipaka ya kazi yao ili kuepuka kudhalilishwa au kuvuruga zoezi hilo.

“Mtu anaenda kumhesabu msanii halafu anapost mtandaoni, walipaswa kwanza wajue mipaka yao ya kazi,” amesema Vida.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika hilo Seleman Bishagazi, amesema hawaungi mkono mtu anayepiga picha na kutuma mitandaoni akilenga kuwadhalilisha makarani wa sensa.

“Makarani wa sensa hasa wanawake wanatafutiwa ‘angle’ ya kudhalilishwa, sisi hatuungi mkono mtu anayepiga picha na kutuma mitandaoni akilenga kumdhalilisha karani,” amesema Bishagazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles