24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Ubunifu wahitimu DIT wamkuna Waziri Ndalichako

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

UBUNIFU wa wahitimu katika mahafari ya 15 ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), umemfurahisha Waziri wa Elimu Sayasi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako ambapo amesema kwa mambo aliyoyaona ni wazi kuwa nchi haipo nyuma kwenye mapinduzi ya nne ya uchumi wa viwanda.

Prof. Ndalichako alikuwa mgeni rasmi katika mahafari hayo yaliyofanyika leo Desemba 2,2021 kwenye viwanja vya chuo hicho, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mafari hayo, ameipongeza taasisi hiyo kutokana na mfumo wao wa utoaji mafunzo na kuitaka kuendelea kuwekeza katika mafunzo ya viwandani (Teaching Factory).

Waziri huyo amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, inategemea zaidi teknolojia katika uchumi wa viwanda, hivyo taasisi hiyo ina wajibu wa kuzalisha wataalamu bora na weledi, wanaokidhi viwango vya Kimataifa.

Amesema hakuna budi kuendelea kujipanga katika ili kuendana na kasi iliyopo na anatambua taasisi hiyo ina wataamu wa kutosha kwa sababu ni ngumu kutenganisha maendeleo ya viwanda na sayansi na ubunifu.

“Rais wetu Samia Suluhu Hassani, amekuwa akisisitiza elimu ya ufundi na kwa kuweka mfano anajenga chuo cha ufundi Dodoma. Kwa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam amewapatia shilingi bilioni 74 kwa ajili ya kuendeleza kituo cha umahiri cha ngozi kampasi ya Mwanza na fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

“Fedha hizi  zipo naomba mharakishe michakato ya manunuzi, vituo hivi vitakapokamilika vinaendeleza kutoa mafunzo kwa vitendo ili wanapohitimu wawe wameiva.

“Sifa kubwa ya mapinduzi ya uchumi wa nne wa viwanda ni teknolojia, nimeona katika maonyesho yenu kuna mambo makubwa mnafanya, mmegusa maeneo yote yanayotakiwa hadi roboti mnatengeneza, kwa utaalamu na ubunifu mlioonyesha hapa nchi yetu haipo nyuma”, ameeleza Prof.Ndalichako.

Aidha amewataka wahitimu wa chuo hicho kwenda kuwa chachu ya kuendeleza utaalamu waliopata kwa manufaa ya Taifa, pia wawe mabalozi wazuri wa taasisi hiyo ambayo imetoa wabobezi wengi katika fani ya uhandishi.

“Ndugu wahitimu nianze kwa kuwapongeza kwa hatua mliyofikia, si kazi nyepesi, nichukue nafasi hii pia kuwapongeza wanafunzi ambao wameamua kuanzisha kampuni zao, ninawapongeza vijana hao kwa uthubutu, naomba huko mnakokwenda mkaendelee kuwa na uthubutu.

“Mkiwa ni wahitimu, mnatambua hazina kubwa ya elimu  ufundi mliyoipata  kwa manufaa  binafsi, jamii na wazazi kwa maendeleo ya Taifa, nina imani mtakuwa chachu katika kuendeleza uchumi wa viwanda na ubunifu,” amesema Prof. Ndalichako.

Naye Mkuu wa chuo hicho, Prof. Preksedis Ndomba, ametaja jumla ya wahitimu kuwa ni 104, wanaume 754 na wanawake 250 ambayo ni asilimia 25.

Prof. Ndomba amesema wamejiimarisha zaidi katika mafunzo ya kutaalam ya kutumia muda mwingi katika vitendo ili kuweza kutoa watu wanaoweza kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

“Pia tumeingia mikataba 30 na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi katika kuendelea kuwapa utaalamu wananfunzi na wahadhiri wetu,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Tasaisi ya DIT, Dk. Richard Masika, amesema kumekuwa na ufinyu wa  mafunzo kwa vitendo, hivyo kuiomba Serikali kuzishawishi taasisi na viwanda kutoa nafasi, pia kujitolea kwenda kufundisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles