Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Benki ya UBA Tanzania imeungana na nchi nyingine za Afrika kushehereke siku ya Afrika kama sehemu ya kumbukumbuku ya kila mwaka ya kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) na sasa Umoja wa Afrika (AU) ambao ulianzishwa Mei 25, mwaka 1963.
Kwa hapa nchini benki hiyo iliadhimisha siku hiyo, Mei 24, mwaka huu kwa wafanyakazi wake kuvaa nguo za mitindo mbalimbali yenye kuonyesha uhalisia wa Waafrika.
Akizungumzia siku hiyo Mkuu wa Kampuni ya Benki ya UBA Tanzania, Mussa Kitambi, amesema kuasisiwa kwa benki hiyo kunajumuisha historia ya Afrika kupitia mavazi, umoja na vyakula vya jadi.
“Siku ya Afrika (zamani ya Uhuru wa Afrika na Siku ya Uhuru wa Afrika) ni kumbukumbu ya kila mwaka ya msingi wa OAU na sasa AU mnamo Mei 25, mwaka 1963.
“Siku hii inaadhimishwa katika nchi mbalimbali katika bara la Afrika, pamoja na duniani kote,” alisema Kitambi.
Katika kukumbuka siku hizi shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwamo kuvunja nazi, kukata keki na wateja, ngoma ya jadi na wafanyakazi, ngoma ya jadi na Kikundi cha Flash.