SANTIAGO, Chile
BINGWA wa zamani wa uzito wa juu duniani, Mike Tyson, amezuiwa kuhudhuria sherehe za tuzo za filamu mjini Santiago, Chile baada ya kujitokeza dosari katika sheria za uhamiaji za nchi hiyo.
Lakini raia huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 51 ambaye aliwahi kufungwa jela kwa ubakaji, unyanyasaji na umiliki wa dawa za kulevya, alirudishwa nyumbani na maofisa wa polisi wa idara ya uhamiaji ya nchi ya Chile.
Maofisa wa polisi katika Uwanja wa Santiago, walisema Tyson alirudishwa nyumbani kwa kufeli kuafiki sheria za uhamiaji.
Tyson alizuiwa kuingia nchini Uingereza 2013 kutokana na matatizo yaliyomkumba wakati wa nyuma.
“Baada ya kutathmini rekodi yake kulingana na sheria za uhamiaji, wageni wote ambao walihukumiwa kwa kutekeleza uhalifu wowote hawaruhusiwi kuingia nchini humu,” walisema polisi.
Bingwa huyo mara mbili alihudumia miaka mitatu jela katika kifungo cha miaka sita 1992 kwa kumbaka mgombea wa shindano la malkia wa urembo nchini humo.
Tyson alikuwa bingwa wa uzito wa juu mwenye umri mdogo katika historia ya mchezo huo wakati alipomshinda, Trevor Berbick, 1986.