26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Trump agoma kuvaa mavazi ya kujikinga na corona, aagiza bendera zipepee nusu mlingoti

 WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump amegoma kuvaa mavazi ya kujikinga na corona wakati alipotembelea kiwanda cha magari.

Rais Trump ambaye alifanya ziara katika kiwanda cha magari ya Ford, hakuvaa mavazi ya kujikinga, licha ya kwamba mwanasheria wa jimbo la Michigan alimuomba kufanya hivyo.

Aidha ameagiza bendera zipepee nusu mlingoti kwenye majengo yote ya Serikali nchini Marekani kama ishara ya kuwakumbuka maelfu ya watu waliofariki kutokana na janga la virusi vya corona nchini humo. Trump amesema katika ujumbe aliouweka kwenye ukurasa wake wa Twitter, kwamba hatua hiyo itakayodumu kwa muda wa siku tatu, italenga kuwakumbuka Wamarekani waliopoteza maisha katika janga la virusi vya corona.

Wakati huo huo zaidi ya watu 660,000 inaelezwa wamepoteza makazi wakati wa janga la corona. 

Shirika la misaada la kimataifa la Norwegian Refugee Council, limesema zaidi ya watu 660,000 wamepoteza makaazi yao katika maeneo yenye migogoro duniani tangu mwezi Machi, licha ya Umoja wa Mataifa kutoa wito wa kusitisha mapigano duniani wakati wa janga la virusi vya corona.

Shirika hilo la NRC, limesema takwimu zake zinaonyesha kuwa migogoro ya kutumia silaha duniani imeendelea wakati wa janga la corona, licha ya vizuwizi vilivyowekwa katika maeneo mengi duniani. Hali imeendelea hivyo licha ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa, Antonio Guterres kutoa wito Machi 23 wa kuwepo na usitishaji wa uhasama duniani.

NRC imesema jumla ya watu laki sita na elfu 61 wamepoteza makazi yao katika mataifa 19 tangu wakati huo, huku idadi kubwa zaidi ikiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles