Na Sussan Uhinga – Tanga
MAMLAKAÂ ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga imekifunga Chuo Kikuu cha Eckern Forde kutokana na madeni ya kodi ya mapato.
Hatua hiyo inatokana na chuo hicho kudaiwa kutolipa madeni hayo ya Ongezeko la Thamani (VAT) pamoja na ile ya mishahara kwa wafanyakazi (PAYE) tangu mwaka 2012 hadi 2016.
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Masawa Masatu, alisema jana kuwa uamuzi huo umechukuliwa  baada ya kubainika kuwa ni wadaiwa sugu wa kodi za TRA.
Alisema taasisi hiyo inamiliki majengo ya shule, shule ya msingi, sekondari,   chuo cha ualimu   na hosteli.
Alipotakiwa kutaja ni kiasi gani cha fedha kinachodaiwa chuo hicho, Masatu alisema   taratibu haziruhusu kutaja deni la mdaiwa kwa mujibu wa sheria.
Alipotafuta Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Kiango, alisema kuwa wao wataendelea na masomo kwa sababu  ni majengo ya utawala ndiyo yaliyofungwa na si madarasa na walimu wataendelea na ratiba zao.