29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

TRA YAIDAI TANESCO BILIONI 4/-

Na PATRICIA KIMELEMETA – DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) linadaiwa zaidi ya Sh bilioni 4 na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) za kodi ya mitambo ya kuzalisha umeme iliyokwama katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mradi wa uzalishaji wa umeme wa gesi asilia wa Kinyerezi, Dar es Salaam, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Deo Ngalawa, alisema kuwa mitambo hiyo iliingizwa nchini ili kuongeza uzalishaji wa umeme.

Alisema hadi sasa mitambo hiyo imekwama baada ya Tanesco kushindwa kulipa deni la kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

“Tanesco inadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 4 na TRA, deni hilo linatokana na kukwama kwa mizigo ya kuzalisha umeme, ikiwamo mitambo na jenereta kutoka nje ya nchi, jambo ambalo linachangia kurudisha nyuma uzalishaji wa umeme,” alisema Ngalawa.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi wa Uwekezaji wa Tanesco, Khalid James, alisema mradi wa Kinyerezi unatarajiwa kuzalisha megawati 240 za umeme, hivyo kupunguza tatizo la upatikanaji wa nishati hiyo.

Alisema mahitaji ya umeme kwa sasa ni megawati 1,700, lakini Tanesco wanazalisha megawati 1,366, kutokana na hali hiyo, kumalizika kwa mradi huo kutasaidia megawati 1,521.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles