Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital
Kampuni ya Tigo Tanzania imezindua Promosheni ya ‘Lipa kwa simu Uwini’ yenye lengo la kuhamasisha wateja wa Tigo Pesa kutumia huduma ya malipo ya kidijitali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumanne Novemba 23, jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa Promosheni hiyo, Afisa Mkuu wa Biashara na Huduma za Kifedhawa Tigo Pesa, Angelica Pesha amesema inalenga kukuza matumizi ya malipo ya Kidigitali nchi nzima hasa kueleka msimu wa Sikukuu za mwisho wa Mwaka.
Amesema kupipia promosheni hiyo watumiaji waote wa Tigo Pesa watapata zawadi za pesa hadi Sh milioni moja, vocha za zawadi ikiwamo kurudishiwa asilimia 10 watakapofanya malipo kwa njia ya simu kwa wafanyabiashara waliosajiliwa kote nchini.
Aidha, amesema wakati huohuo wamedhamiria kuwazawadia wateja wao waaminifu katika msimu huu wa sikukuu kwa kila malipo watakayofanya kupitia huduma ya Lipa Kwa Simu na Tigo Pesa ambapo watapata nafasi ya kujishindia zawadi za fedha taslimu, punguzo la asilimia 10 katika maeneo yaliyochaguliwa na zawadi za Vocha.
“Kila mteja atakayeshiriki atapokea ofa kwa njia ya SMS inayomtaka kufikia idadi au kiwango fulani cha miamal’ a kupitia Lipa Kwa Simu kulingana na wastani wa matumizi yake ya kila wiki, akifikia namba ya lengo aliyotengewa mteja atapata zawadi ya Vocha kuanzia Sh 2,000 hadi Sh 100,000 kwenye akaunti yake ya Tigo Pesa papo hapo na wateja 10 bora tu ambao wataongoza kwa kutimiza lengo kwaasilimia 50 watapata zawadi ya Vocha ya Sh 100,000 kila wiki,” amesema Pesha.