27.7 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

The Desk and Chair Foundation yachangia vifaa kuokoa wajawazito

Na Sheila Katikula, Mwanza

Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania yenye makao makuu yake jijini Mwanza, Sibtain Meghee, ametoa msaada wenye thamani ya Sh milioni 7.5 ikiwemo vifaa 184 vya kujifungulia akina Mama,  baskeli za watu wenye ulemavu mbili na mahema matano.

Mkurugenzi wa Shirika la The Desk and Chair Sibtain Meghee (kushoto) akikabidhi vifaa vya kusaidia watu wenye ulemavu na wajawazito kwa mkuu wa wilaya ya Ilemela Dk.Severine Ralika katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. Picha Na Sheila Katikula, Mwanza. 

Msaada huo ulitolewa juzi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani vifaa vya kujifungulia wakina Mama vilikabidhiwa kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa ya Sekou Teure.

Meghee alisema lengo la kutoa msaada huo ni kuhakikisha wakina mama wa vijijini ambao hawana uwezo wanajifungua  salama   kwenye vituo vya afya pindi wanapohitaji huduma hiyo.

Alisema  kwenye maadhimisho hayo taasisi hiyo imetoa msaada wa baskeli mbili  kwa watu wenye ulemavu zenye thamani ya Sh 120,0000  ili kuhakikisha  wanazitumia waweze kufika  kwenye shughuli zao za kila siku.

“Tumetoa msaada wa   baskeli mbili kwa watu wenye ulemavu, viburudisho vikiwamo maji, Juice na biskuti kwa   kituo cha damu Salama kanda ya ziwa wenye thamani ya sh 50,0000 ili mtu anayechangia damu aweze kupewa viburudisho.

“Vile vile tumechangia  kuweka mahema matano yenye thamani ya Sh 450000 na vifaa 184 vya kujifungulia wakina mama ambavyo watapewa bure watu ambao hawana uwezo wanaoishi vijijini pindi watakapoenda kwenye vituo kijufungua  watavikuta hap,”alisema Meghee.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Angela Benedictor, ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Serikali la Wote Sawa linalojishughulisha na utetezi wa haki za wafanyakani wa nyumbani amewataka waajiri wa kike kuacha kuwanyanyasa wasaidizi wa kazi  za nyumbani ili waweze kuweka usawa kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema wanawake  katika uongozi   ni chachu kufikia dunia yenye usawa.

Naye  Ofisa Mchunguzi Mwandamizi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, Maua Ally, akizungumza kwa niaba ya taasisi hiyo alisema  katika kampeni ya vunja ukimya kataa rushwa ya ngono kila mwanawake  anapaswa kujituma, kujiamini ,kujiheshimu  na kuwajibika  ili kuweza kupinga vitendo hivyo.

“Rushwa ya ngono ni  changamoto katika sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye shule za Msingi,sekondari, makazini na vyuoni  taasisi hii inashughulika na kuzuia na kupambana na vitendo hivi ndiyo maana tumekuja na Kampeni ya vunja ukimya kataa rushwa ya ngono kwani tunaelimisha jamii ili iweze kutambua madhara yake.

“Tunataka kuhakikisha pindi anapokutana na  tatizo hili aweze kutoa taarifa na uchukua hatua za kumfikisha mahakamani mhusika  wa kitendo hicho  kwani  tunaimani kila mama akijiheshimu,  
Kujiamini, kuwajibika  hatoweza kufumbia macho suala hili,”alisema Mauwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles