26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

THABEET APATA TIMU JAPAN

Kanto region, japan

Nyota wa zamani wa kikapu wa okc thunder ya ligi kuu ya marekani (nba), mtanzania hasheem thabeet, amefanikiwa kujiunga na timu ya yokohama b corsairs ya ligi kuu nchini japan.

Mchezaji huyo mara ya mwisho alikuwa anacheza katika ligi d ndani ya klabu ya grand rapids drive ya nchini marekani, lakini kwa sasa amejiunga na klabu hiyo ya nchini japan huku dau la usajili wake hadi sasa halijawekwa wazi.

Thabeet mwenye umri wa miaka 30, amekabidhiwa jezi yenye namba 34 ambayo alikuwa anaitumia tangu akiwa kwenye timu ya memphis grizzlies, dakota wizards, houston rockets, oklahoma city thunder na nyingine.

Mchezaji huyo alitamba na kuitangaza tanzania kupitia mchezo huo mara baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi kuu ya nba nchini marekani katika msimu wa 2009 akiwa na timu ya memphis grizzlies.

Hata hivyo, alikuja kufanya vizuri akiwa na timu ya oklahoma city thunder katika msimu wa 2012 hadi 2014, lakini baada ya hapo kiwango chake kilionekana kushuka kwa kiasi kikubwa na hatimaye kupelekwa kwenye ligi ya maendeleo ili kuweza kurudisha kiwango chake na kutafuta nafasi ya kurudi ligi ya nba.

Nyota huyo anatarajia kuonekana kwenye ligi hiyo ya nchini japan ‘b-league’ ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi leo hii, hivyo inaweza ikawa ni nafasi yake mchezaji huyo kuonesha uwezo wake na kurudi katika ligi ya nba nchini marekani.

Yokohama b corsairs ni miongoni mwa timu ambazo zina maendeleo makubwa kwenye kikapu nchini humo, kwa kuwa ilianzishwa mwaka 2010, lakini inafanya vizuri kwenye michuano ya ligi kuu.

Wadau mbalimbali wa kikapu wameonekana kufurahia hatua hiyo ya thabeet kupata nafasi ya kucheza tena ligi kuu nje ya marekani kwa kuwa ataweza kulitangaza taifa la tanzania kwenye mataifa mengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles