26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

TFDA yabaini kiwanda bubu cha dawa bandia

picha-no-1

Na Judith Nyange,

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa imebaini kiwanda bubu cha dawa bandia katika mji  mdogo wa Buselesele wilayani Chato Mkoa wa Geita.

Kiwanda hicho kilichofanya kazi tangu mwaka 2008 pia hutengeneza vifungashio vya dawa  zilizokwisha muda wa matumizi   na kutengeneza lebo mpya za dawa.

Kiwanda hicho kimegundulika katika nyumba moja ya makazi inayodaiwa kumilikiwa na mwananchi mmoja (jina tunalo)  wakati maofisa wa TFDA Kanda ya Ziwa walipofanya ukaguzi wilayani humo.

Mkaguzi wa dawa wa TFDA, Venance Bulushi, alimweleza Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Selestine Gesimba kuwa walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuhusu  nyumba  hiyo ndipo walipoamua kufuatilia.

“Tulifika kwenye nyumba hiyo tukaona hakukuwa na dalili yoyote ya mtu kuishi ndani yake.

“Tuliondoka eneo hilo  tukamwacha mtu maalum wa kufuatilia kwa siri  nyumba hiyo, baada ya dakika 30 yule mtu alitupigia simu kuwa ile nyumba imefunguliwa na kuna maboksi yanatolewa na kupelekwa nyumba jirani.

“Tuliporudi na kuingia ndani tulikuta dawa nyingi ambazo zimekwisha muda wake wa matumizi na vifungashio vyake zenye uzito tani mbili  na  thamani ya Sh milioni 71.

“Taarifa tulizozikuta ndani ya chumba hicho zinaonyesha kazi hiyo imekuwa ikifanyika tangu 2008,” alisema Bulushi.

Alisema vitabu vya stakabadhi vinaonyesha mtu huyo amewahi kusambaza dawa maeneo ya Bunda, Ngara, Kibondo, Shinyanga Runzewe, Mwanza na baadhi ya vituo vya afya na zahanati za shule za sekondari .

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Selestine Gesimba, aliwataka watumishi wa Halmashauri za Geita    kujitathimini kwa sababu haiwezekani wakaguzi watoke Mwanza wafike na kubaini kiwanda hicho wakati  wao  hawana taarifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles