Tunu Nassor, Dar es Salaam
Tume ya vyuo Vikuu Tanzania(TCU), imefungua dirisha la udahili kwa awamu ya nne utakaoanza Oktoba mosi hadi 4, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 25, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema lengo ni kutoa fursa kwa wananchi ambao hawakuweza kuahiliwa katika awamu tatu kupata nafasi hiyo.
Amesema tume imepokea maombi pia kutoka kwa vyuo ambavyo bado vina nafasi kuhitaji kuongezwa muda wa udahili.
“Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua dirisha la udahili kwa awamu ya nne utakaoanza Oktoba mosi hadi 4,mwaka huu,” amesema profesa Kihampa.
Amevitaka
vyuo vyote vya elimu ya juu kubainisha proramu zenye nafasi ili kuwawezesha
waombaji kufanya maamuzi sahihi wakati wa kutuma maombi ya udahili.
Amewakumbusha waombaji wote kuwa masuala ya yanayohusiana na udahiliama
kuthibitisha yawasilishwe moja kwa moja katika vyuo husika na si TCU.