Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Dunia wa Ufugaji Nyuki (APIMONDIA) utakaofanyika mwaka 2027 nchini wadau wametakiwa kutumia fursa kwa kuvutia wawekezaji na kuongeza tija katika ufugaji na biashara .
Hayo yameelezwa SeptembA 12 jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) ameseme mkutano huo unatarajia kuwa na washiriki 6,000.
Amesema kupitia mkutano huo wadau wa ufugaji nyuki wajitokeza kwa wingi kwani utatoa fursa mbalimbali ikiwemo kuvutia wawekezaji na kuongeza tija katika ufugaji na biashara nzima ya mazao ya nyuki na utalii.
“Tumieni mkutano huu vizuri kwa kuongeza tija katika ufugaji na biashara nzima ya mazao ya nyuki, kuongeza wigo wa mashirikiano na taasisi mbalimbali duniani katika kuvutia uwekezaji katika sekta hiyo pamoja na kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za ufugaji nyuki hususani teknolojia na mbinu mbalimbali za kuboresha na kuendeleza sekta hii,” amesisitiza Kairuki.
Ametoa wito kwa Watanzania na wadau mbalimbali kuwekeza katika sekta hiyo kwa kuwa kwa sasa uzalishaji wa asali ni tani takribani 32,000 tu wakati kama taifa kuna uwezo wa 138,000.
Amesema mkakati wa Serikali ujulikanao kama “Achia shoka kamata mzinga” ambao umelenga kudhibiti ukataji wa miti ovyo na badala yake kujikita katika kuongeza mizinga.
Akizungumzia nafasi ya nchi duniani Kati uzalishaji wa nyuki amesema Tanzania ni nchi ya 14 duniani na ya pili Afrika katika uzalishaji wa asali bora.
Aidha, amesema kuwa kwa Tanzania kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa APIMONDIA Tanzania inakwenda kuwa nchi ya pili Barani Afrika kupewa jukumu hilo kubwa la kuandaa kongresi hiyo tangu kuanzishwa kwa APIMONDIA miaka takribani 130 iliyopita.
“Kwa mara kwanza Kongresi hiyo kufanyika Barani Afrika ilikuwa mwaka 2001 ilipofanyika nchini Afrika ya Kusini,”amesema
Amefafanua kuwa mkutano huo unakadiriwa kushirikisha wadau zaidi ya 6,000 toka mataifa mbalimbali dunia hivyo Tanzania kuwa mwenyeji wa kongresi hiyo kunatarajiwa kuleta manufaa makubwa ya kuchochea ukuaji wa sekta ya nyuki na uhifadhi, kuongeza mchango wa sekta katika pato la taifa, kuchochea utalii kwa ujumla nchini na kuvutia uwekezaji wa viwanda na teknolojia katika sekta ya ufugaji nyuki.
Ushindi wa Tanzania ulitangazwa na Rais wa APIMONDIA, Jeff Pettis mbele ya wajumbe waliohudhuria shughuli za kuhitimisha mkutano mkuu wa 48 wa Shirikisho hilo uliomalizika nchini Chile.
“Ushindi huu ni hatua muhimu kwa Tanzania kama nchi lakini pia kwa Bara zima la Afrika kwani unakwenda kuwakutanisha wataalamu mbalimbali wakiwemo wafugaji nyuki duniani wafanyabiashara, wasomi, watafiti pamoja na wachakataji wa mazao ya nyuki,” ameongeza.
APIMONDIA ni Shirikisho la Umoja wa Vyama vya Wafugaji nyuki Duniani lililoanzishwa mwaka 1895 nchini Italia huku Tanzania ilijiunga katika shirikisho hilo mwaka 1984 ambapo Tanzania kwa mwaka huu nchini Chile iliibuka kuwa mshindi wa kinyanganyiro cha kuandaa Mkutano wa 50 na mwaka 2027 ni Tanzania