27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU FEKI WAKAMATWA  KWA RUSHWA IKULU

 

Na Walter  Mguluchuma -MPANDA

TAASISI ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Katavi, imewatia mbaroni watu wawili kwa tuhuma za kupokea rushwa.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi, John Minyenya aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Nicodemo Peter na Peter   Mwaninsawa,    wote ni wakazi wa Mtaa wa Nsemlwa   Manispaa ya  Mpanda.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakipokea rushwa ya Sh 400,000 nje ya jengo la Ikulu ndogo Mkoa wa Katavi, kwa kujifanya wao ni maofisa wa Takukuru.

Minyenya alisema watuhumiwa hao walikamatwa jana     asubuhi baada ya kuwekewa mtego huo baada ya kupata taarifa kutoka kwa msiri wao juu ya watu hao waliokuwa wakijiita ni maofisa wa Takukuru Kitengo cha Uchunguzi.

Alisema   kabla ya  kukamatwa kwa watuhumiwa hao walimpigia simu msiri wa  Takukuru wakidai kuwa wana jalada la uchunguzi dhidi ya msiri huyo.

“Kutokana na hali hiyo watu hao walimtaka msiri wetu awape Sh 400,000  waweze kulifunga jalada kwa  kufuta tuhuma zilizomkabili msiri huyo  ambaye ni   Mtendaji wa  Kijiji  cha Vikonge  wilayani   Tanganyika.

“Walidai alikuwa akituhumiwa kupokea  rushwa ya kutoka  kwa wafugaji  ambao alikamata  mifugo yao na kuiachia  baada ya kupokea rushwa ya Sh milioni 2.5.

“Msiri wetu huyo ambaye hapendi na anapinga rushwa alilazimika  kufika ofisi ya  Takukuru na kutoa taarifa juu ya  maofisa hao bandia wa Takukuru na tulipowekewa mtego tulifanikiwa kuwatia mbaroni leo (jana),” alisema Minyenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles