24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Stars na kiapo cha moto kwa Farao

ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

HADITHI nyingi za kale zimesimuliwa ndani ya nchini ya Misri lakini zinaweza kuwa tofauto na hii ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), ambayo itaanza Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu nchini humo.

Katika michuano hiyo zipo timu zimefuzu baada ya kupita miaka mingi kama ilivyokuwa kwa timu ya Taifa Stars ambayo kwa mara ya kwanza imefanikiwa kupenya tangu mwaka 1980.

Nyingine ni Madagascar ambayo imefuzu michuano hiyo baada ya kupita miaka 15  wakati Burundi ikifuzu kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mshindano hayo  kuanzishwa mwaka 1957.

Misri itafungua michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mafuta ya Total kwa kucheza dhidi ya Zimbabwe katika kundi A ambako pia kuna timu za Leopards ya Jamhuru ya Demokrasia Kongo na Uganda ‘The Cranes’.

Mafalao wamekuwa wenyeji baada ya kuipiku  nchi ya Cameroon.Hii itakuwa mara ya tano kwa nchi hiyo kuwa wenyeji wa mixchuano hiyo Afrika.

Mara ya mwisho  kuwa wenyeji ilikuwa mwaka 2006  na mwaka huo walifanikiwa kunyakua ubingwa pia waliweza kulitetea taji hilo  m,waka 2008 katika michuano iliyochezwa nchini Ghana pia ilishinda tena ubingwa wa taji hilo mwaka 2010 ilipofanyika nchini Angola.

Nchi  hiyo iliwahi kutwaa michuano hiyo mwaka 1959, 1974 na  1986. Mwaka huu idadi ya timu zimeongezeka  kutoka 16 hadi 24.

Tanzania imepangwa kundi C katika michuano hiyo ikiwa pamoja na Kenya, Algeria na Senegal.Taifa Stars itachezea mechi zake katika Uwanja wa Juni 30 na Al Salam iliyopo mjini Cairo, Misri.

Kundi D linaundwa na Namibia, Afrika Kusini, Ivory Coast na Morocco, wakati Kundi E kuna Angola, Mauritania, Mali na Tunisia na Kundi F ni Guinea Bessau, Benin, Ghana na mabingwa watetezi, Cameroon. 


Taifa Stars ilifuzu baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi L kwa pointi zake nane, nyuma ya jirani zao wa Afrika Mashariki, Uganda walioongoza kwa pointi zao 13 wakizipiku Lesotho iliyomaliza na pointi sita na Cape Verde pointi tano.    

Mwaka huu, Tanzania itashiriki AFCON kwa mara ya pili tu kihistoria baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria ambako ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji, Nigeria, Misri na Ivory Coast na kushika mkia.


Mwaka huo ilifungwa mechi mbili, mabao 3-1 dhidi ya Nigeria na  mabao 2-1 dhidi ya Misri kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Ivory Coast na kuishia raundi ya kwanza wakati huo zikishiriki timu nane tu katika michuano hiyo.   

Safari hii Taifa Stars inakwenda Misri ikiwa na hamasa inayochagizwa na viongozi pamoja na wananchi wanaopenda mchezo wa soka.

Imani kubwa ipo nyuma yao tena safari hii ikiwa na zaidi ya wananchi milioni 50 tofauti na ilivyokuwa awali.Hii inaweza kuwa chachu ya mafanikio ya Taifa Stars.

Lakini kitendo cha Serikali kuwapa zawadi ya viwanja na sh  milioni 10 wachezaji hao ni mafano tosha kuwa kila Mtanzania yupo nyuma yao.

Jukumu walilopewa Taifa Stars kwenda kulifanya nchini Misri ni kama kula kiapo cha utiifu kwamba lazima wafuzu hatua inayofuata baada ya makundi.

Ni kweli timu hiyo ipo katika kundi gumu ambalo linaonekana kuwa na ushindani makali lakini katika dhana ya ishindani ili uwe timu bora lazima ushindane na timu bora.

Katika mchezo wa soka lolote linawezekana jambo muhimu ni maandalizi maana hakuna aliyesahau kilichotokea Novemba  mwaka 2015 zile bao 7-0 kutoka Algeria ambao tupo nao tena katika kundi.

Lakini kila kitu kimebadilika hata wachezaji katika kikosi cha Stars pia kocha anayewafundisha sasa ni Mnigeria Emanuel Amunike badala ya yule Boniface Mkwasa ambaye alikuwapo siku hiyo tunalambishwa mabao 7-0 bila kujibu.

Ni vema pia Stars wakakumbuka kiapo walichoapa pale Ikulu mbele Rais John Magufuli kwamba wataendelea kupambana na kulipa heshima Taifa.

Wanatakiwa kufahamu hiki ni kipindi cha kuweka heshima kama ambavyo wameiweka ya kufuzu hatua ya m,akundi kwenye michuano hiyo hivyo ni jukumu lao pia kuhakikisha wanafanya vizuri kwa mara nyingine lakini si kuathirika na majina makubwa ya nchi walizopangwa nazo.

Hakuna mwanzo mwepesi katika mapambano kila kitu kinahitaji juhudi na maarifa pia maandalizi ya dhati kama Kamati, wadau pamoja na wachezaji watafahamu wajibu wao kuhakikisha timu hiyo haiteteleke kwenye michuano hiyo.

Ni fahari  ya kila Mtanzania kuona timu hiyo inavuka hatua nyingine katika michezo ya awali ya makundi kwa matumaini ya kufika mbali na kuweka rekodi na pengine hata kunyakuwa ubingwa wa michuano hiyo.

Kocha Amunike bado anaonekana mwenye tamaa ya kutaka kuisaidia timu hiyo kuweka rekodi na kuandika hadithi mpya akiwa na Mbwana Samatta, Simon Mzuva, John Bocco na Himid Mao.

Pengine hii ndio nafasi pekee ya Jonas Mkude,Salum Feisal na Gadie Michael kuweka kumbukumbuka katika vizazi vyao.

Hiki kinaweza kuwa kiapo cha moto kwao  wakitamani majina yao kuandikwa mbele ya vizazi vyao.

Katika kipindi chao mchezo wa soka umekuwa maarufu kuliko michezo yote nap engine ndio unaoongoza kuleta faraja katika maisha ya Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles