27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

St. Joseph yafadhili wanafunzi wawili kusoma Italia

MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

CHUO Kikuu cha St. Joseph Dar es Salaam kimetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wawili kwenda katika Chuo cha Parma nchini Italia kusomea Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Uhandisi wa Mawasiliano.

Akizungumza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wakati akiwasindikiza wanafunzi hao, Makamu Mkuu wa Chuo cha St. Joseph, Profesa Innocent Ngalinda, alisema hatua hiyo ni mipango ya chuo hicho ambayo pia ni ushirikiano na vyuo vingine vingi duniani.

Alisema masomo hayo ni mchakato na  mipango ya Tanzania kujiandaa kurusha satelaiti.

“Wengine tutawapeleka Ulaya, watakwenda kusoma masuala ya umeme na India, na kama mnavyofahamu India ndiyo nchi ya kwanza kurusha satelaiti na hiyo ndiyo mipango ya chuo kwa sasa,” alisema.

Mmoja wa wanafunzi hao, Frank Charles aliwashauri wanafunzi ambao bado wako shuleni kujitahidi katika masomo yao na kuwa na malengo kwamba wanataka kuwa nani.

“Ukiwa na malengo unaweza kufanikiwa, kama mimi binafsi nilijiwekea malengo kwamba lazima nifikie shahada ya uzamili na kwa muda fulani na nashukuru Mungu imeweza kunifikia kwa muda sahihi, nawashauri wanafunzi wenzangu kujitahidi, changamoto najua zipo cha msingi ni kumuomba Mungu azidi kutuimarisha,” alisema.

Penina Mbwilo ambaye naye anakwenda Italia, alisema siku zote alikuwa akitamani akimaliza masomo ya shahada ya kwanza aendelee na shahada ya pili kwa hiyo hii nafasi imekuja wakati mwafaka.

“Ujumbe wangu kwa wanafunzi wenzangu ni wasome tu na kujiongeza katika masomo na shughuli mbalimbali za darasani, kuwa na malengo, nidhamu na utii.

“Lengo ni kupata ujuzi na nikipata ujuzi nisikae nao peke yangu, niwafundishe wenzangu nao waelimike,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles