28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

SHULE YA USA RIVER YAKATIWA UMEME KWA WIZI

Shule ya Usa River Academy iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha imekatiwa umeme baada ya  mmiliki wa shule hiyo, Robert Lukumay kubainika kuchezea Mita za Luku ili kutumia umeme wa bure

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali mkoani hapa, Ofisa wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Kitengo cha Udhibiti Mapato Makao Makuu, Bupe Mwakyanjala amesema, timu hiyo iko mkoani Arusha ili kukagua endapo wateja wao wanatumia umeme kwa halali na kama miundombinu ya umeme ipo salama.

“Tukiwa katika zoezi la ukaguzi, tulifika eneo ilipo Shule ya Usa River Academy huyu ni mteja wetu anayemiliki shule mbili moja ya msingi na nyingine ya sekondari na tumekuta akiwa amefunga mita mbili tofauti, moja upande wa sekondari na nyingine shule ya msingi, ambapo ndani ya mita hiyo amekata baadhi ya waya muhimu ili apate umeme bila kulipia.

“Mita iliyokuwa imefungwa upande wa Shule ya Sekondari haikuwa ikitumika zaidi ya kutumia mita ya Shule ya Msingi ambayo nayo alikuwa akitumia umeme bure,” amesema.

Naye Ofisa Mkaguzi wa shirika hilo, Mhandisi Hussein Mbulu akifafanua zaidi amesema wakiwa katika ukaguzi huo kwa upande wa nyumba ya makazi ya mmiliki wa shule hizo walibaini pia kuwapo kwa mita tatu, ambapo mita moja ilikuwa ikitumia kwa ajili ya mashine, nyumbani na stoo.

“Mita nyingine katika eneo hilo la makazi zilikuwa sawa, kasoro mita iliyokuwa nyumbani kwake tumekuta akiwa ameichezea mfumo wa kupunguza umeme unaoweza kutumika kwenye mita,” amesema Mhandisi Mbulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles