30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano yafanyika kila mkoa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kilele cha sherehe za Maadhisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mwaka huu yamefanyika kiaina yake, ambapo kila mkoa unaadhimisha kwa kutelekeza maelekezo mahsusi ya Serikali.

Mkurugenzi wa Kitengo ya Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Batholomeo Jungu ameyamesema hayo leo Aprili 26, wakati ziara maalum ya Kamati ya Kitaifa ya maadhimisho hayo mwaka huu ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa maelekezo mahsusi kwa Ofisi za Serikali jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Kitengo ya Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Batholomeo Jungu akitoa maelezo wakati wa ziara ya timu ya wataalam katika Jengo la Ofisi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ikiwa ni ziara ya timu hiyo kukagua namna Ofisi za Serikali zilivyotekeleza maelekezo mahsusi ya namna ya kuadhimisha Miaka 59 ya Muungano jijini Dodoma.

Jungu alisema kuwa kwenye mikoa ndipo kwenye wananchi hivyo shughuli hizi kufanyika katika mikoa zinaleta chachu ya uzalendo kwa wananchi sababu kila mtu anapata nafasi ya kushiriki kuanzia kwenye uzinduzi wa miradi, mashindano ya insha kwa wanafunzi, michezo mbalimbali, usafi wa mazingira na maswala mengine muhimu.

“Watu wapo katika kila mkoa, hivyo tukio hili la kushirikisha wananchi linaleta tija kwa jamii kwa kuona ni sehemu ya maadhimisho haya kwa vitendo,”alisisitiza Jungu.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mary Maganga alisema.

Kila mwaka Aprili 26, hututumika kama kumbukumbu ya sherehe za Muungano wa Iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, uliyofanya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo kaulimbiu ya Mwaka huu inasema: “Umoja wetu na Mshikamano ndiyo nguzo ya kukuza uchumi wetu.”

Katibu Mkuu Masanja alitumia fursa hiyo kueleza namna ofisi yake ilivyotekeleza maelekezo mahsusi ikiwemo kulipamba jengo la ofisi hiyo na kuweka picha za viongozi wakuu wa nchi pamoja na waasisi wa taifa leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles