27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YACHUKUA MASHAMBA YA MKE WA SUMAYE, JEETU PATEL

Serikali imefuta umiliki wa shamba la ekari 473, lililokuwa linamilikiwa na mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, Esther Sumaye na mengine manne ya eka 2,661 ya Kampuni ya Noble Agriculture Enterprises Limited, inayomilikiwa na mfanyabiashara Jeetu Patel baada ya kushindwa kulipia kodi.

Mashamba hayo, ni miongoni mwa mashambapori mengine 14, yenye ukubwa wa zaidi ya eka 14,341 yaliyokuwa yanamilikiwa na watu mbalimbali wilaya za Kilombero, Mvomero na Kilosa, mkoani Morogoro.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema mashamba pori hayo yamefutwa kutokana na wamiliki wake kushindwa kulipa kodi za ardhi na kuyaendeleza.

“Maelekezo ya rais baada ya kufuta mashamba hayo ni kumtaka Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya mkoani hapa kuhakikisha mashamba hayo yanasimamiwa vizuri katika ugawaji hasa kwa kuzingatia watu wenye mahitaji ambao wapo jirani na mashamba hayo,” amesema Lukuvi.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Lukuvi amewaonya viongozi wenye nia ya kujipenyeza kwa lengo la kuchukua maeneo kwenye mashamba hayo na kwamba wale watakaojipenyeza watajulikana na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles