26 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaanza utekelezaji wa ahadi ya barabara ya Chepuo

Na Mwandishi wetu, Ludewa

Serikali imeanza kutekeleza ujenzi wa barabara ya Chepuo kwa kiwango cha lami yenye urefu wa KM 1.2 iliyoko Mlangali wilayani Ludewa mkoani Njombe ikiwa ni ahadi ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa ziara ya kuomba kura wilayani humo mwaka jana.

Akikagua zoezi la upimaji linaloendelea tayari kwa kuanza ujenzi huo jana, mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga, ameiomba serikali kuharakisha mchakato wa manunuzi kutokana na hali ya mvua katika mkoa wa Njombe na kwamba itakapokamilika itawanufaisha wananchi kiuchumi.

‘’Jimbo hili ni lenye idadi kubwa ya watu huu ni mji mkongwe wa siku nyingi una kituo cha afya ambacho kinafanya upasuaji kabisa watu hawaendi tena kutafuta huduma za uzazi mbali, kwa hiyo hii barabara itasaidia pia wagonjwa kwenda kwenye kituo cha afya kwa urahisi,”alisema Kamonga.

Upande wao wananchi wa jimboni humo akiwemo, Maria Mtitu, amesema barabara hiyo awali ilikua na mashimo ambayo yalikua yakisumbua katika usafirishaji ambapo mitikisiko ilikua mingi na kupelekea hata wajawazito kujifungulia njiani.

Naye, Furaha Mwinuka amesema wanafarijika kuona Mkandarasi ameanza upimaji kwa ajili ya kuanza ujenzi huo kwani wanaamini itakuwa muarobaini wa uchumi.

‘’Muda mrefu walisema wataleta barabara lakini sasa tumeona utekelezaji kwa sababu wameanza kupima ikiwa nzuri itatusaidia kukuza vipato vyetu kwa kusafirisha mizigo pamoja na kushuka kwa nauli,” amesema Furaha.

Kwa upande wake Afisa Tarafa ya Mlangali, Alsenus Mtweve, amesema Serikali imesikia kilio cha wananchi wake kwa kuanza zoezi la ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ambayo itainua uchumi na kukuza vipato vyao.

Naye, Christopher Mpenda ambaye ni Mhandisi kutoka kampuni ya ujenzi ya Kipera amesema barabara hiyo yenye urefu KM 1.2 inatarajia kukamilika ifikapo juni mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles