29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI YA KENYA YAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO

NAIROBI: Kenya


SERIKALI ya Kenya imepiga marufuku maandamano katika miji mitatu mikubwa ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.

Waziri wa Mamo ya Ndani, Fred Matiang’i  alisema hatua hiyo ni katika kuwalinda wananchi wa Kenya na mali zao.

Wafuasi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakiandamana mara kwa mara katika miji hiyo, hali ambayo imekuwa ikisababisha uporaji na mapigano na polisi.

Viongozi wa upinzani wanataka yawepo marekebisho muhimu kwa Tume ya Uchaguzi (IEBC) kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio wa urais baadaye mwezi huu.

Mwanzoni mwa wiki hii, Kiongozi wa upinzani wa muungano wa Nasa, Raila Odinga alijiondoa katika kinyang’anyiro hicho.

Mahakama Kuu ilifuta ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa awali uliofanyika Agosti mwaka huu, baada ya kuilaumu IEBC kwa kukiuka taratibu na mwenendo wa uchaguzi na sheria zake.

Matiang’i alisema hatua ya kupiga marufuku maandano haina maana kuwanyima wananchi uhuru wao wa katiba lakini umechukuliwa tu baada ya maofisa usalama kuona kuwa kuna “hatari mbele”.

Alisema amepokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara kuhusu athari za maandamano hayo kwa shughuli zao.

Alisema pia kuwa viongozi wakuu wa Nasa ndiyo watawajibika kwa uharibifu wowote uliotokana na maandamano ya juzi.

Nasa kimewataka wafuasi wake wafanye maandamano ya mara kwa mara kuibana IEBC ifanye marekebisho yanayotakiwa kabla ya uchaguzi huo wa marudio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles