25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuimarisha sheria za kazi kwa kufanya kaguzi

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha mwaka 2021/22 serikali itaimarisha utekelezaji wa sheria za kazi kwa kufanya kaguzi katika maeneo ya kazi kwa kutoa elimu na ushauri kwa wafanyakazi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 13, 2021 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya ofisi yake kuelekea mwaka wa fedha wa 2021/22.

Amesema hadi kufikia Februari, mwaka huu jumla ya kaguzi 4,771 za viwango vya kazi zimefanyika sawa na asilimia 99.4 ya kaguzi 4,800 ambazo zilikuwa zimepangwa kufanyika.

“Aidha, kaguzi 110,123 zilizohusu afya na usalama mahali pa kazi zimefanyika, kufuatia kaguzi hizo waajiri 1,162 walichukuliwa hatua kali za kisheria.

“Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kazi na wafanyakazi kwa kusimamia viwango vya kazi na wafanyakazi pamoja na afya na usalama mahali pa kazi,” amesema Majaliwa na kuongeza kuwa:

“Katika kipindi cha mwaka 2021/22 serikali itaimarisha utekelezaji wa sheria za kazi kwa kufanya kaguzi katika maeneo ya kazi kwa kutoa elimu na ushauri kwa wafanyakazi.

“Pia waajiri na vyama vyao, lengo hapa ni kueleza namna bora ya kutekeleza sheria hizo, kuimarisha majadiliano ya pamoja baina ya waajiri na wafanyakazi pamoja na serikali lakini pia ushirikishwaji wa wafanyakazi katika maeneo ya kazi kupitia mabaraza ya wafanyakazi ili kuboresha maslahi,” amesema Majaliwa.

Kaguzi mbalimbali katika maeneo ya kazi zimekuwa zikitekelezwa na na OSHA ambayo ni taasisi ya serikali iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu ambayo husimamia utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles