Amina Omari, Muheza
Serikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya kilimo na masoko ili kumuhakikishia mkulima soko la mazao wanayozalisha.
Ahadi hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, wakati akiongea na wananchi wa kijiji cha Sakale kilichopo wilayani Muheza kwenye ziara yake ya kata kwa kata kukagua shughuli za maendeleo.
Amesema wakati serikali inaendelea na kuboresha mazingira ni jukumu la wakulima kuendelea kuongeza uzalishaji wa mazao yao.
Nao wakulima wa mazao ya viungo katika Kijiji hicho waliiomba serikali kuwasaidia kutafuta soko la uhakika wa mazao hayo ikiwemo bei elekezi ili waweze kunufaika na kilimo hicho.
Mmoja wa wananchi hao Michael Simon amesema kuwa wanalazimika kutembea umbali za zaidi ya Kilomita 9 kufata soko la mazao yao.