29.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuanzisha maeneo ya usindikaji mazao ya mifugo

Anna Potinus

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Wizara ya Mifugo imeunda kikosi kazi kinachoangalia uwezekano wa kuanzisha maeneo madogo madogo ya usindikaji wa mazao ya mifugo.

Bashe amesema hayo leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Alfredina Kahigi aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani kuzuia wafugaji wasigonge mihuri ngozi ili wasikose soko na wana mkakati gani wa kuwatafutia wafugaji vifaa vya kuwekea maziwa yao kwakuwa vifaa wanavyovitumia sio bora.

“Kwa kuwa wafugaji wanakamua maziwa mengi je serikali ina mkakati gani wa kuwatafutia vifaa vya kuwekea maziwa yao kwani vifaa wanavyovitumia sio bora,” amehoji.

Akijibu swali hilo Bashe amesema serikali itachukua hatua ya juu ya fursa ya uwepo wa maziwa mengi kutoka kwa wafugaji.
“Wizara ya Mifugo imeunda kikosi kazi ambacho kinahusisha Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mifugo na Wizara ya Fedha.

“Kikosi kazi hiki kinaanza kuzunguka kuangalia uwezekano wa namna gani ya kuanzisha maeneo madogo madogo ya usindikaji wa mazao ya mifugo hasa maziwa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles