24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuanzisha Benki ya DNA kupambana na uhalifu

Mwandishi Wetu, Dodoma

Serikali imeanza mchakato wa uanzishwaji wa mfumo rasmi wa Kanzidata ya Taifa ya Vinasaba vya Binadamu (DNA) ambayo itasaidia kuwatambua wahalifu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema hayo bungeni akijibu kwa maandishi swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest (Chadema), aliyetaka kujua mkakati wa serikali kutengeneza Benki ya DNA kama mkakati wa kupunguza uhalifu kwa kuwa ni rahisi kupata watuhumiwa kwani Benki ya DNA itasaidia kulinganisha na watakaohisiwa.

Amesema wizara kwa kushirikiana na Taasisi nyingine imeandaa andiko la dhana ya uanzishwaji wa Kanzidata hiyo (DNA Database Concept Note) na mpango kazi wa utekelezaji (Road Map) kwa kushirikiana na wataalamu wazalendo wa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) nchini kutoka Taasisi za Serikali ikiwemo Wakala wa Serikali Mtandao (eGA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Ufilisi na Udhamini (RITA) na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

“Aidha, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, imeandaa utaratibu wa kushirikisha wadau wengine muhimu wakiwemo vyombo vya Ulinzi na Usalama ili kupata maoni yao yatakayosaidia katika uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo huo wa kanzidata hiyo na mfumo huu utaanza kutekelezwa baada ya taratibu hizo kukamilika,” amesema Ummy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles