Leonard Mang’oha, Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya amewataka wanachama, wapenzi na Watanzania kwa ujumla kutorudi nyuma katika kudai haki na usawa kwa wote.
Ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Januari 27 wakati wa kumbukizi ya miaka tisa ya vurugu zilizotokea Januari 26 na 27 mwaka 2001 visiwani Zanzibar, baada ya wananchi kuandamana wakidai Tume Huru ya Uchaguzi na kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba kutokana na kasoro zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000.
Sakaya amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1992 hakijawahi kurudi nyuma katika kudai haki.
“Pamoja na shuruba mbalimbali tunazozipata hatutarudi nyuma katika kudai haki kwa wote.
“Leo tunaona katika taifa ambalo tunadai tuna demokrasia vyama vya upinzani haviruhusiwi kufanya mikutano lakini viongozi wa chama tawala wanaendelea na mikutano sehemu mbalimbali nchini,” amesema Sakaya.