25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Riek Machar arejea Juba baada ya miaka miwili

JUBA, SUDAN KUSINI



KIONGOZI wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar amerejea katika mji mkuu Juba jana, ikiwa ni  mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili ili kushiriki katika sherehe ya utekelezaji wa mkataba wa amani.

Machar ambaye chini ya makubaliano yaliyofikiwa ya amani atarudishiwa wadhifa wa makamu wa rais, hakuwa amekanyaga mjini hapa tangu alipokimbia Juni 2016 kutokana na makabiliano makali wakati mwafaka wa awali wa amani uliposambaratika.

Kiongozi huyo aliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Juba jana asubuhi na kulakiwa na Rais Salva Kiir, mshirika wake wa zamani aliyegeuka kuwa adui.

Viongozi hao walijumuika na wengine wa kikanda katika sherehe iliyofanyika baadaye jana ya kuyakaribisha makubaliano ya amani yaliyofikiwa mjini Addis Ababa, Ethiopia Septemba mwaka huu.

Msemaji wa chama cha Machar cha SPLM-IO, Lam Paul Gabriel alisema kiongozi huyo ameandamana na viongozi karibu 30 wa kisiasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles