26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

RC Makalla awaonya watumishi wanaochochea migogoro ya ardhi Mwanza

Na Clara Matimo, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CPA Amos Makalla amewaonya watumishi wa idara ya ardhi wanaosababisha migogoro ya ardhi kwa wananchi na kusema kwamba hawana nafasi ndani ya mkoa huo kwa kipindi chote cha uongozi wake.

CPA Makalla ametoa onyo hilo jijini Mwanza leo Desemba 8, 2023 wakati akifungua kikao cha Bodi ya Ushauri ya Mkoa huo (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi yake.

Baadhi ya wadau walioshiriki kikao cha RCC mkoa wa Mwanza.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza amebainisha kwamba tangu alipoanza kazi mkoani humo Septemba 18, 2023 alizindua zoezi la kusikiliza na kutatua kero za wananchi zilizo ndani ya uwezo wake ambapo hadi sasa ameishatatua migogoro ya ardhi 454 katika wilaya zote za mkoa wa Mwanza alizozunguka na kugundua kwambva kero zingine zinasababishwa na maafisa ardhi wasiowaadilifu katika utumishi wao.

“Katika ziara yangu ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi ndani ya wilaya zote nimegundua kwamba kero zingine zinasababishwa na maafisa ardhi ambao wanagawa viwanja mara mbili, mwananchi anakuwa amekwishamilikishwa kiwanja halali lakini akija mwenye pesa naye wanampa hicho hicho kiwanja hivyo wanatengeneza mgogoro,

“Niseme kwa kipindi changu cha uongozi ndani ya mkoa huu maafisa ardhi wa namna hiyo hawana nafasi ndani ya mkoa wangu, Septemba 18 nilipozindua zoezi la kusikiliza na kutatua kero za wananchi niliwaagiza viongozi wote wa Wilaya nao kufanya hivyo maana viongozi tusipotoka kwenda kuwasikiliza wananchi watanyimwa haki kwa kuwa maafisa ardhi wengine ni waongo, nataka niwaambie watumishi wa serikali tukawasaidie wananchi tusisababishe migogoro,” ameagiza CPA Makalla.

Baadhi ya wadau walioshiriki kikao cha RCC mkoa wa Mwanza.

Aidha, CPA Makalla amesema azimio la mkoa wa Mwanza ni kufufua zao la pamba ili Mkoa huo uwe kinara katika uzalishaji wa zao hilo na kuongeza malighafi katika viwanda pamoja na kuweka mikakati ya kuhakikisha wavuvi wanafanya uvuvi halal ili kuinua uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo,

Awali akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja alishauri mambo matano ambayo ni kuhakikisha mkoa huo unajitosheleza kwa chakul, ,kuongeza mapato, kufufua zao la pamba, kuweka mikakati kwa ajili ya kukuza utalii na kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ili kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anayetoa fedha kwa kila halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

“CCM tutatoa ushirikiano mkubwa kwa ngazi zote kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya hadi kata ili kuhakikisha mambo hayo yanafanikiwa, Wabunge endeleeni kupaza sauti kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ili wananchi wajue pia wasisitizeni wautunze ili idumu muda mrefu,” ameshauri Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles