VICTORIA, SHELISHELI
RAIS wa Shelisheli, James Michel, ametangaza atajiuzulu siku chache baada ya chama chake kushindwa kwenye uchaguzi wa wabunge.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 72, amekuwa madarakani tangu mwaka 2004 na chama chake kimetawala taifa hilo la visiwa kwa miongo minne.
Alitoa tangazo hilo la ghafla kupitia runinga siku ya Jumanne ambapo aliahidi kuondoka madarakani ifikapo Oktoba 16.
“Baada ya kuhudumu miaka 12 kama rais, wakati wangu kukabidhi madaraka kwa kiongozi mpya umewadia. Kiongozi mpya ataifikisha Shelisheli katika hatua nyingine ya ufanisi.”