26.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS WA GHANA AKUMBWA NA KASHFA YA WIZI WA HOTUBA

Rais mpya wa Ghana, Nana Akufo-Addo
Rais mpya wa Ghana, Nana Akufo-Addo

ACRA, GHANA

OFISI ya Rais mpya wa Ghana, Nana Akufo-Addo, imelazimika kuomba radhi baada ya hotuba ya rais huyo aliyoitoa wakati wa sherehe za kuapishwa kwake, kuonyesha baadhi ya mistari imeibwa kutoka hotuba za marais wa zamani wa Marekani.

Muda mchache baada ya kiapo hicho Jumamosi, baadhi ya watumiaji mitandao ya jamii na vyombo vya habari vikubwa mjini hapa vilianza kufananisha baadhi ya mistari ya Akufo-Addo na hotuba zilizowahi kutolewa na marais Bill Clinton na George Bush.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais, Eugene Arhin, alikiri wizi huo na kuomba radhi, hasa kwa kunakili maandishi hayo pasipo kumnukuu mwandishi wa awali.

Hata hivyo, hilo halikumfanya awe salama baada ya Ikulu kumtimua kwa kosa hilo la kuifedhehesha ofisi hiyo ya juu kabisa nchini hapa.

Rais huyo aliapishwa Jumamosi iliyopita akiahidi kuongeza ajira, kutokomeza umasikini, kukuza biashara na kuirejesha Ghana katika nafasi ya taifa lenye nguvu kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles