25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mkumbo afanya ziara kwenye mradi wa Magadi Monduli

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amefanya ziara katika Mradi wa Magadi soda uliyopo kata ya Engaruka wilayani Monduli mkoani Arusha itakayo gharimu Sh billioni mia 400, na kupitia mradi huo tayari mikakati imeshaanza ya ulipaji fidia kwa wananchi watakaopisha mradi huo pamoja na muwekezaji .

Mradi huo mkubwa ni mmojawapo ya miradi muhimu iliyowekwa kwenye Mpango wa Miradi ya Maendeleo ya miaka mitano, 2020-2021 mpaka 2025-26 na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Prof. Mkumbo amesema kuwa wilaya ya Monduli imebahatika kutoa mojawapo ya miradi mikubwa ambayo inatarajiwa kutekelezwa ndani ya miaka mitano ya Rais Sami.

Waziri Mkumbo amesema pia ili mradi huo uanze kuna hatua 3 za kufuata ambazo amezitaja kuwa ni upembuzi yakinifu, kupata mwekezaji na kusimamia mikataba.

“Maana yake ulipaji fidia kwa wanachi wote 599 watakaopisha mradi huu takribani Sh billioni 14, Jumla ya Hecta 25,115 na vipaombele kwa wanufaika wa mradi huu ni wananchi wa Engaruka halmashauri ya Monduli,” amesema Prof. Mkumbo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo, Fredrick Lowassa, aliyekuwa mwenyeji katika ziara, amemshukuru Waziri Mkumbo kwa kufanya ziara jimboni kwake na kutoa rai kwa wananchi na viongozi wa eneo hilo na Monduli kwa ujumla kujikita zaidi katika manufaa wa Mradi huo katika Kuleta Maendeleo.

Dk. Yohana Mtoni ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Viwanda Mama -NDC amesema kulinga na upembuzi yakinifu wingi wa Magadi ni mita za ujazo takriban Billioni 3.3, na uzalishaji wake unatarajiwa kwa kuanzia tani laki tano (500,000) kwa mwaka, tofauti na ukilinganisha na nchi za jirani kama Kenya 300,000, Botswana 300,000. Lakini wakubwa duniani ni Uturuki million 3.5 na Marekani million 9.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles