30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WAMKAMATA  MBUNGE MTWARA

Na FLORENCE SANAWA – MTWARA

JESHI la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema) kwa tuhuma za uchochezi.

Awali mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kusini, aliwasili kituoni hapo saa 6.00 mchana kwa ajili ya mahojiano.

Alikwenda kituoni hapo akiwa na Mratibu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Tambwe Hiza   na mawakili wa Kampuni ya Phoenix Advocates.

Mahojiano hayo na polisi yaliyodumu zaidi ya saa tano yalichukua sura mpya baada ya mbunge huyo  kuwekwa ndani wakati akisubiriwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mtwara,   Ronald Makona ambaye hakuwapo kituoni hapo.

Akizungumza   kituoni hapo, Tambwe alisema   hatua ya kumkamata mbunge huyo inaweza kufifisha kampeni za udiwani ambazo zilipangwa kufanyika kesho katika Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi.

Kuhusu hoja ya uchochezi, alisema  katika  mkutano wa uzinduzi wa kampeni wa Kata ya Reli mkoani Mtwara hakukuwa na viashiria vyovyote vibaya kwa kuwa ulikuwapo usalama wa kutosha.

“Jana tulifika mkutanoni tulimaliza salama lakini tukiwa njiani kwenda Tandahimba mbunge alipigiwa simu na polisi wakimuhitaji.

“Lakini yeye aliwaahidi leo ndiyo ameafika lakini hadi sasa hatuoni dalili ya kuachiwa kwake,” alisema.

Mwanasheria wa Kampuni ya Phoenix Advocates, Rainery Songea alisema polisi wanadai mbunge huyo alitamka maneno ya uchochezi wakati wa uzinduzi wa kampeni katika Kata ya Reli Manispaa ya Mtwara Mikindani.

“Kimsingi wanamhoji kwa tuhuma za uchochezi ambazo wanasema jana akiwa kwenye kampeni za udiwani Kata ya Reli kuna maneno alitamka ambayo yanaweza kusababisha   wananchi kufanya makosa,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya hakuweza kupatikana kutoa ufafanuzi wa suala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Uongozi wa ccm na polisi kwa sasa uchunguzwe na kuchukuliwa hatua.kazi za polisi ni kuleta na kutunza amani na usalama wa wananchi. Hapa naona polisi wameenda ubia naccm kunyanyasa na kuvunja amani Tanzania.Tatizo ni uongozi wa nuu wa ccm kutokuheshimu mipaka ya sheria za nchi. Hii ni hatari kwa taifa zima. Kama raisi hanitambui afanyalo. Iwe makusudi. Woga au kutokujua afanyalo pia achukuliwe hatua kwani anapeleka nchi hii kubaya sana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles