25.6 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi afukuzwa kazi kwa kumtorosha mtuhumiwa

NA SAMWEL MWANGA, SIMIYU

JESHI la Polisi, Mkoa wa Simiyu, limemfukuza kazi askari polisi mmoja kwa tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa wa mauaji.

Pia, askari wengine saba mkoani hapa wanaendelea kushikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kuwatorosha watuhumiwa watatu wa mauaji na ujangili waliotoboa ukuta wa chumba cha mahabusu hivi karibuni na kutoroka wilayani Meatu.

Taarifa hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Kamanda Lyanga alimtaja askari polisi aliyefukuzwa kazi kuwa ni mwenye namba za usajili, F3817, PC Benjamin aliyekuwa akifaya kazi katika Kituo cha Polisi Luguru, Wilaya ya Itilima.

Kwa mujibu wa Kamanda Lyanga, mtuhumiwa aliyetoroshwa na polisi huyo alifahamika kwa jina la Kwandu Maduhu.

“Februari 27 mwaka huu, katika Kituo cha Polisi Lugulu, askari mwenye namba F 3817 PC Benjamin, alimtorosha mtuhumiwa wa
kesi ya mauaji, Kwandu Maduhu (70), mkazi wa Kijiji cha Gambasingu, wilayani Itilima.

“Kwa hiyo, huyo askari amefukuzwa kazi kwa sababu amelitia aibu Jeshi la Polisi na atafikishwa mahakamani wakati wowote.

“Katika lile tukio la kutoroka kwa watuhumiwa wa ujangili wilayani Meatu, tunaendelea kuwashikilia askari saba wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo.

“Kwa kifupi ni kwamba, watuhumiwa hao waliotoroka siyo waliohusika kutungua helkopta na kusababisha kifo cha rubani Rogers Gower, raia wa Uingereza kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti.

Kuhusu askari wanaoshikiliwa baada ya watuhumiwa hao kutoroka, Kamanda Lyanga aliwataja kuwa ni mwenye namba D 5582 Koplo Peter, mwenye namba F9840, anayeitwa Husein, mwenye namba G4806 PC John na mwenye namba G8602 PC Yassin.

“Wengine ni mwenye namba  WP 11257 PC Khadija, mwenye namba G8371 PC Adam na askari mwingine mwenye namba za usajili H8410 PC Kher,” alisema Kamanda Lyanga.

Watuhumiwa hao wa ujangili, walitoroka  Januari 19 mwaka huu, majira ya usiku wakiwa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Meatu mkoani hapa.

Waliotoroka ni Chiluli Sitta (28), mkazi wa Kijiji cha Mwasungula aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji. Wengine ni Paschal Masanja (18) na baba yake, Masanja Ndegule (45), wote wakazi wa Kijiji cha Sapa ambao walikuwa wakituhumiwa na umiliki wa meno ya tembo kinyume cha sheria.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles